

Tangu lilipoanzishwa, shirika la Green Crescent limekuwa likipambana
na utumiaji madawa ya kulevya nchini Uturuki na kwingineko duniani
katika harakati zake za kutunza heshima na neema ya binadamu.
Tulijadili miradi ya kitaifa nay a kimataifa ya shirika la Green Crescent na
Rais Prof. Dr. Mücahit Öztürk ambayo ni msingi ambao unatekeleza kazti
zake kwa kuzingatia jukumu hili wakati wote.
Tangu kuanzishwa, shirika la green
Crescent limekuwa na mnapambano
makali dhidi ya aina zote za kulewa.
Tafadhali simulia safari yauanzishaji
wa shirika la Green Crescent.
Kulewa ni shida kubwa duniani kote
na yenye athari hasi za kimwili na
kiakili kwa mtu binafsi, na ambayo
huleta madhara kwa jamii mbalimbali
na kudhoofisha uchumi wa kitaifa.
Licha ya kuwa na ujuzi wa madhara
ya madawa ya kulevya, aina za vilevyo
na idadi ya walevi inazidi kuongezeka
nchini Uturuki na kwingineko duniani.
Hili linatuonyesha kwamba maadili ya
kibinadamu yanazidi kuzoroteka, na
mahusiano ya kibinadamu yanazidi
kudhoofika, na pia kwamba kulewa
madawa kumefika kilele. Inadhihirisha
pia kwamba katika karne ya 21, jamii
zitajitahidi kujilinda dhidi ya kulewa
madawa kwa namna yoyote ile.
Shirika la Green Crescent lilianzishwa
mwaka wa 1920 na wataalm sifika
waliokuwa na kipaumbele cha ukubwa
wa shida hii karne moja iliyopita, na
wakatafuta njia ya kuzuia ukuaji wa
kutumia madawa ya kulewa wakati
na baada ya vita. Mapambano haya,
ambayo mwanzoni yalikuwa dhidi
ya kulewa pombe, yamepanuka
baadaye
kuzingatia
pia
sigara,
madawa na kamari, na hivi juzi,
ulevi wa kiteknolojia umeongezwa
kwenye orodha hii. Tangu wakati
huo, viongozi, maafisa na watumishi
wote wa shirika la Green Crescent
wamebeba bendera ya mapambano
haya adimu, wameendeleza kazi na
shughuli za shirika hili wakiwa na
jukumu hili nyoyoni na wamejitahidi
sana kuhakikisha kwamba jukwaa hili
adimu liko imara. Pia, wanatafuta njia
na nafasi za kusambaza mapambano
haya duniani kote na kuhakikisha
yanaendelezwa,
kwa
kuwezesha
ufahamu kwamba kulewa ni shida
yenye athari hasi kwa binadamu wote.
Kwa kusaidiwa na mashina ya kitaifa
ya shirika la Green Crescent, zaidi ya
mashina 100 nchini Uturuki, pamoja
na wafanyakazi na watumishi wa
kujitolea, shirika la Green Crescent
linabeba bendera ya vita dhidi ya
kulewa.
Picha ni za: Semih Akbay
PROF. DR.
MÜCAHİT ÖZTÜRK:
“UTUMIAJI MADAWA
YA KULEVYA
NI SHIDA KUBWA
KOTE DUNIANI”
Prof. Dr. Mücahit Öztürk alipata digri
kutoka chuo kikuu cha Hacettepe, Ndaki
ya Elimu Tiba mwaka 1990. Katika mwaka
1997, alimaliza masomo yake ya uzamivu
katika Chuo Kikuu cha Istanbul, Ndaki ya
Elimu Tiba, Idara ya Afya na Maradhi ya
Kichwa ya Watoto na Ushauri wa Watoto,
mwaka 1990. Alipandishwa cheo kuwa
Profesa Mshiriki mwaka 2000 na kisha
akawa Profesa mwaka 2007, na hivi sasa
ameajiriwa katika Idara ya Saikolojia ya
Chuo Kikuu cha Hasan Kalyoncu. Baadhi
ya machapisho yake ni pamoja na School
Phobia katika jarida ka Kurasa 99 (2006),
Ushauri wa Watoto (2007), Watoto wa
Wazazi Waliotengana (2008) na Wasiwasi
Katika Watoto (2015). Prof. Dr. Mücahit
Öztürk ni Rais wa sasa wa shirika la Green
Crescent.
PROF. DR. MÜCAHİT ÖZTÜRK NI NANI?
4