

Kampeni iliyozinduliwa na Green Crescent chini
ya kauli mbiu; “Nina sababu”, inayolenga kuvuta
mapambano dhidi ya uraibu, inapata msaada
kutoka kote duniani. Watu kutoka nchi na
tamaduni tofauti ambazo huwasiliana na Green
Crescent hujiunga na kampeni yetu ya “Nina
sababu” kuelezea kwa nini wanahusika katika
vita dhidi ya ulevi katika lugha zao za mama,
wakilenga kuchangia juhudi za uhamasishaji wa
hatari za uraibu katika kiwango cha kimataifa.
9