

Crescent kawaida linalinganishwa
na shirika la Msalaba Mwekundu na
shirikisho lake la Red Crescent kwa
misingi ya utaratibu wake na kazi
zake, ingawa ulinganisho huu huwa
si halisi kabisa. Kutokana na aina
za kazi zake, mashirika haya mawili
hushirikiana sana na mamlaka za
kiserikali na hufanya kazi zake kwa
kufuata majukumu yake wakati wa
vita na wakati wa amani. Kutokana
na mtazamo huu, shirika la Green
Crescent la Uturuki na Shirikisho la
Kimataifa hutofautiana ma mashirika
yale. Kwa kuwa tuna upekee duniani,
inatuwezesha kupiga hatua mbele
katika ngazi ya dunia, lakini kwa
kuwa hatuna mfano wa kuiga,
lazima tuwe watangulizi wa kila kitu.
Tunapokumbana na tatizo, tunajitetea
na kueleza nia yetu, jambo ambalo
linatufunguliamilango na kusuluhisha
matatizoya kila aina.
Kama Shirikisho, wanachama wenu
mnawasaidiaje? Mnatoa miradi
gani? Tafadhali zungumzia usaidizi
ambao mnatoa.
Kama Shirikisho, tunajaribu kusaidia
wanachama wetu kwa namna yoyote
ile katika ngazi ya dunia. Lengo
la muhimu zaidi la mashina ya
Green Crescent ya nchi mbalimbali
yaliyochini ya Shirikisho hili ni kuinua
uwezo. Usaidizi wetu kwa miradi
unatofautiana kulingana na sifa,
tamaduni, watu, itikadi na mbinu za
msingi zinazofaa kutumika katika
vita dhidi ya ulevi katika nchi binafsi.
TunatakakilanchiiwenashinalaGreen
Crescent, na kwa kila shina la kitaifa la
Green Crescent, liwe na uwezo uleule
kama wa shirika la green Crescent
la Uturuki. Lengo letu ni kuanzisha
mashina ya mataifa ambayo yataamua
sera kuhusu ulevi katika nchi zao,
ambazo zinatawala kazi za kukinga
dhidi ya ulevi na kutoa huduma za
kukarabati walevi kulingana na uwezo
wake. Ulevi ni tatizo linalowanda kwa
haraka, na kwa hiyo nchi zote ziko
hatarini. Kwa sababu hii, mashina ya
kitaifa yanatakiwa kupigana vita vikali
dhidi ya ulevi ili kulinda jamii zao na
nchi nyinginezo dhidi ya janga hili.
Kama Shirikisho, tunatoa usaidizi
wa kutekeleza miradi katika mipaka
ya Mipango ya Kimataifa ya Misaada
ya Kifedha ili kuimarisha uwezo wa
mashina ya kitaifa na kuchangia
harakati zao. Kupitia Mpango
wake wa Kimataifa wa misaada ya
Kifedha, shirika la Green Crescent
linataka
kuhakikisha
kwamba
mashina ya kitaifa yanatekeleza kazi
endelevu, yanaimarisha uwezo wake,
yanachangia sera za ulevi za kieneo
na kujenga miundo-mbinu yake ya
utetezi. Pia tunayahimiza mashina ya
kitaifa kushiriki kwenye kazi za utetezi,
utafiti wa kisayansi na uchunguzi
wa jinsi ya kutoa kinga dhidi ya ulevi
katikanchi zao, nakuanzishamitandao
ya kitaifa na kimataifa. Mpango wetu
wa Kimataifa wa Misaada ya Kifedha
wa 2020 utaanza kutekelezwa mwezi
wa Januari 2020. Tunaandaa mpango
wa Kuinua uwezo wa Mashina ya
kitaifa ya Green Crescent kila mwaka
ili kuinua uwezo wa mashina ya nchi
mbalimbali. Pia tunaandaa mazoezi
ya mafunzo ya uwezo, ambapo
tunasisitiza mahitaji ya mashina ya
kitaifa ya Green Crescent kuhakiki
aina za ulevi zilizopo katika nchi zao.
Tunashirikiana katika kuamua ni aina
zipi za ulevi ambazo ni za hatari Zaidi
katika nchi husika.
Mwisho kabisa, tunafikiria namna
ya kutekeleza Mpango wa Mafunzo
ya Kuzuia Ulevi wa Uturuki; mpano
ambao unalenga kuzuia tabia ya ulevi,
au mipango mingine katika nchi
nyinginezo.
Dunia imefika daraja gani katika
vita dhidi ya ulevi, na tunaweza
kufanya nini?
Ninaamini kwamba vita dhidi ya
ulevi vimepiga hatua mbele kutokana
na mchango mkubwa wa shirika
la Green Crescent duniani kote.
Tunaamini kwamba, kuanzia harakati
za kuzuia hadi kutoa masuluhisho,
ulegevu wowote usitokee katika vita
dhidi ya ulevi. Ingawa ulimwengu
unapendelea sera za kusulusisha
kuwa ndizo mwafaka zaidi katika
vita dhidi ya ulevi, sisi tuna mtazamo
tofauti. Nchi zinazotekeleza sera
za usuluhishaji hatimaye zitageuza
mtazamo na kuunga mkono mkabala
wetu wa pamoja dhidi ya ulevi.
Wakati wa Mkutano wa Miradi wa
Istanbul uliokuwa jijini Istanbul na
kuhudhuriwa na mashirika 21 kutoka
nchi 15, tulikumbusha dunia tena
kuhusu umuhimu wa utafiti wa kinga
katika vita dhidi ya ulevi. Kutokana
na mkutani huu, tuliona kwamba
kuna nchi nyingi zinazounga mkono
mkabala wa pamoja katika vita dhidi
ya ulevi.
Kama Shirikisho, lazima tusambaze
harakati zetu za kupambana na
ulevi kwa kila upembe za dunia kwa
ukakamavu na bila kuchoka wala
kukata tamaa. Matatizo ya ulevi
hayawezi kutatuliwa kwa muda
mfupi. Katika miaka 15 ijayo, tutakuwa
tunashika mikono ya watoto na
vijana ambao wanapewa mafunzo ya
kuwawezesha kujiepushanaulevi sasa,
na watatushika mikono na kukimbia
kuelekea ujao wenye nuru. Tumeingiza
kundi kubwa la watu wenye nguvu na
mawazo mapya katika mapambano
yetu dhidi ya ulevi nchini Uturuki
na duniani kote.Lakini, kwa kuwa
makampuni yanayoshiriki biashara ya
kulevya wanapata hela nyingi, wao hivi
sasa wanajitahidi kushawishi watoto
na vijana kushiriki ulevi. Tunatakiwa
kusimama imara na kupambana na
mambo haya. Tutaendelea kupambana
na ulevi kwa kushirikiana na wengine
duniani kote, bila ya kusaliti ukweli wa
kisayansi.
12