

Shirikisho hili linafanya kazi zake
katika nyanja gani duniani kote?
Pia twambie kuhusu malengo na
mstakabali wa shirikiso hili.
Shirikisho inachukua malengo na
kauli ya mstakabali wake kutoka
shina la Green Crescent la Uturuki,
tofauti ikiwa tu kwamba Shirikisho
ni la kimataifa. Shina la Uturuki
lilianzishwa kwa kutegemea sheria
za Uturuki, na hujishughulisha na
kukinga na kukarabati walevi nchini
Uturuki katika vita vyake dhidi ya
ulevi wa sigara, pombe, teknolojia na
Kamari. Shirikisho hili, kwa upande
wake, linaunga mkono shughuli hizi
za Green Crescent duniani kwa kupitia
wanachama wake, yaani, Mashina ya
kitaifa ya Green Crescent. Lakini, kwa
mtazamo wa Shirikisho hili, hakuna
tofauti kati ya shina la Green Crescent
la Uturuki na mashina mengine ya
kitaifa ya Green Crescent. Hata hivyo,
mashina yote ya Green Crescent
yanajitegemea.
Kama shirika kubwa lenye mtandao
wa
kimataifa,
Shirikisho
hili
linashirikiana na mashina ya Green
Crescent ya kitaifa ili kuratibu kazi
zake, kwa kutegemea majibu ya
maswali kama: kuna ulevi wa aina
gani katika nchi mbalimbali? Ni mbinu
gani zinanoweza kutumiwa kupigana
dhidi ya aina hizo za ulevi? Je, mbinu
zilizofaulu katika nchi moja zinaweza
kutumiwa pia katika nchi nyingine?
Ni tafiti zipi zinazoweza kufanyika kwa
pamoja na mashina ya Green Crescent
ya Kitaifa? Ni masuala yapi ambayo
yajadiliwe kwenye makongamano ya
kimataifa?
Shirikisho lina mkabala gani
wa ushirikiano wa kitaifa na
kimataifa?
Shirikisho halijakuwa, na halina nia
ya kuwa mwanachama wa shirika
lolote la kimataifa. Haiwezekani kwa
shirikisho litakalotenda kazi katika
zaidi ya nchi 100 hivi karibu kuanza
kufanya kazi zake chini ya shirika
lolote. Shirikisho hili linashirikiana
na mashirika yote katika nchi yoyote
ambayo wanachama wake wana
ushirika. Kwa hiyo, kwa mtazamo wa
shirika la Umoja wa Afrika, Umoja wa
Ulaya na Umoja wa dunia, Shirikisho
hili linashirikiana na Shirika la Ulinzi
na Ushirikiano barani Ulaya, na Shirika
la Kusini Pasifiki kupitia mashina ya
Green Crescent ya kitaifa. Shirikisho
hili
linaweza
kushirikiana
na
mashirika yakimataifamengine, lakini
kamwe halitakuwa mwanachama au
kufanya kazi zake chini ya mwavuli wa
mashirika mengine.
Shirikisho hili lina mchango na
nafasi gani duniani katika vita dhidi
ya ulevi?
Ninaamini kwamba dunia inahitaji
huduma za shirika la Green Crescent
la Uturuki kutokana na mkabala wake
wa pamoja katika vita dhidi ya ulevi.
Hakuna shirika lingine duniani ambalo
limeweza kupanuka haraka kama hili.
Maendeleo haya yamesababishwa na
uwezo wa Green Crescent kutanguliza
misingi ya kisayansi katika kazi zake,
na pia kwamba kuna haja ya mkabala
wa pamoja katika vita dhidi ya ulevi
katika kila upembe wa dunia. Katika
kila nchi, tunapata ushabiki mkubwa
kutoka ofisi za juu, kutoka marais
na maafisa wa serikali, na kutoka
mashirika yasiyo ya kiserikali na vyuo
vikuu, wakati tukianzisha mashina
ya Green crescent. Tunafanikiwa hivi
kwa sababu tunaheshimu kila nchi
na kila mtu bila ya kubagua. Sababu
nyingine muhimu ya kuungwa mkono
ni kwamba Green Crescent inatumia
utafiti na miradi vya kisayansi katika
kupigana dhidi ya ulevi, mkabala
ambao unapendwa sana na nchi
nyinginezo. Isitoshe, shirika la Green
Crescent na kazi zake zinatambuliwa
na mashirika ya sifa kama Umoja wa
Mataifa (UN). Kuona kwamba Shirika
la Green Crescent la Uturuki ni shirika
la kimataifa pia ni sababu nyingine
inayotusaidia kuungwa mkono.
Shirikisho hili lilianzishwa chini
ya usimamizi wa shirika la Green
Crescent la Uturuki, likiwa na lengo
kuu la kuinua uwezo wa mashina
ya kitaifa ya green Crescent katika
kila nchi ambako tunapambana na
ulevi. Shirikisho hili bado linaongoza
usambazaji wa mkabala wetu wa
pamoja katika vita dhidi ya ulevi,
kwa kuhakikisha kwamba mashina
ya
kitaifa
ya
Green
Crescent
yanashirikiana katika kupambana na
aina zote za ulevi duniani kote, kwa
kutenda kazi kwa ushupavu na bila
kulegea.
Shirikisho hili lina wanachama
kutoka nchi nyinginezo. Mnawezaje
kupambana na ulevi wakati
mkishirikiana na nchi zilizo na
hitilafu nyingi sana?
Jambo la kutatanisha ni kwamba nchi
zinaainishwa kwa kutegemea uchumi
wake, kiwango cha maendeleo au
aina ya utawala. Lakini, tunakaribisha
wote kwa kutumia mkabala wa kiutu,
kwa kujishughulisha na matatizo ya
watu wengine na bila ya kuzingatia
uainishaji wake. Hii ndiyo sababu
tunapewa heshima katika nchi zote na
tunapokea maneno ya kutusifu katika
mapambano yetu. Shirika la green
Crescent linasifika kote duniani, jambo
linaloonyesha nafasi na mchango wa
Shirikisho hili, na pia kutuonyesha
jinsi tumegusa nyoyo za idadi kubwa
ya watu.
Shirikisho hili lina kifani duniani?
Hakuna shirikisho au shirika la
kimataifa duniani ambalo linapigana
na ulevi kwa kutumia mkabala
wa pamoja. Isitoshe, Shirikisho la
kimataifa na shirika la Green Crescent
ndiyo mashirika ya kwanza kufanya
hivyo duniani. Shirika la Green
Misingi ya Shirikisho hili ina
mizizi yake kwenye shirika
la Green Crescent la Uturuki,
shirika kongwe Zaidi na
lililoimarika Zaidi duniani
katika vita dhidi ya ulevi.
Hivi leo, Zaidi ya mashina
ya Green Crescent ya kitaifa
yanatekeleza kazi zake chini
ya mwavuli wa Shirikisho hili.
Shirikisho hili lina lengo la
kuratibu mashina ya Green
Crescent ya Kitaifa katika
nchi mbalimbali duniani kote,
kupasha tajriba na ujuzi wake,
na kupambana na ulevi duniani
kote kwa kutumia mkabala wa
pamoja na kutegemea ushahidi
wa kisayansi.
11