

Katika miradi yake yote, shirika
la Green Crescent linashirikiana
na wananchi wa Uturuki na
watu kutoka nchi nyingine
kuwashugulisha katika vita dhidi
ya madawa ya kulevya. Mkakati
huu wa Green Crescent unaleta
manufaa gani, hasa katika kuzuia
kulewa?
Tunaamini kwamba njia tu ya kulea
vizazi vyenye afya na uzima ambavyo
tunavitamani ni kuhakikisha kwamba
kila mtu, kutoka umri wa miaka 7 hadi
77, anashirikishwa katika vita hivi.
Ushiriki wa rika zote katika jamii, hasa
vijana, kwenye vita dhidi ya kulewa ni
jambo la muhimu sana kwetu. Katika
mkabala huu, tunalenga kushirikisha
vijana,
wanariadha,
wasanii,
wanahabari, viongozi wa kijamii na
watuwenye sifakatikamiradi yakitaifa
nay a kimataifa tunayounda katika
mapambano yetu dhidi ya kulewa.
Kwa mfano, kupitia Mashindano ya
Vigorogosi ya Kimataifa ya Green
Crescent,
tulishirikisha
wachora-
vigorogosi waliosifika duniani katika
vita vyetu dhidi ya kulewa, na kwa
kutegemea mashindano ya Kizazi
chenye Afya, na Ujao weney Afya,
tuliweza kuhamasisha wanafunzi wa
shule za awali, shule za msingi na
shule za sekondari kuhusu manufaa
ya kushikilia mienendo inayokuza
afya nzuri. Shughuli za vilabu kama
kama chama chanhu: Green crescent,
vilabu katika vyuo vikuu na kampu
za maskauti vimewafanya watoto
na vijana kuwa washiriki muhimu
katika vita dhidi ya kulewa. Kusema
kweli, kama ilivyo kwingineko, vita
bila ushirika, mchango na msaada
wa watu huwa havifaulu. Nina Imani
kwamba tutafaulu katika mapambano
yetu dhidi ya shida hii iliyo ngumu na
yenye changamoto zakila aina kwa
kutegemea vile tutakavyowashirikisha
watu kutoka kila upembe wa dunia.
Katika ngazi ya kimataifa, shirika la
Green crescent ina msimamo gani
kuhusu vita dhidi ya kulewa? Na
unaweza kuelezea uhusiano wake
na mamlaka mbalimbali katika vita
vyake dhidi ya kulewa? Shirika la
Green Crescent linataka kutumiza
nini siku za usoni duniani?
Ningependa
kuwakumbusha
tena
kwamba Green crescent ni shirika
lisilo la kiserikali ambalo lilianzishwa
kwa kipaumbele imara wakati shida
ya kulewa ilikuwa haijadiliwi kirasmi.
Pia ikumbukwe kwamba tumepanuka
sana katika harakati zetu za kutumia
na kuwezesha ukusanyazi wa maarifa.
Tumechukua
hatua
kubwa
kutambulisha vita vyetu dhidi ya
kulewa kimataifa na kuchukuwa
nafasi ya uongozi duniani. Hatua
muhimu Zaidi katika vita hivi ilikuwa
ni kuunganisha mashina ya kitaifa
ya Green Crescent ili kupanua
mapambano yetu dhidi ya kulewa
katika nchi mbalimbali duniani chini
ya mwavuli wa shirika moja. Hatua
hii ilituwezesha kupambana na
kulewa katika nchi za mbali, kutoka
Afrika hadi ulaya, na kutoka Marikani
kaskazini kwenda Asia Mashariki.
Huwa tunasaidia shughuli za kuzidisha
idadi na utendaji bora kazi wamashina
ya kitaifa ya Green Crescent. Wakati
tukisimulia tajriba na ujuzi wetu kwa
nchi nyinginezo, tunaendelea kupanua
vita vyetu dhidi ya kulewa kufikia watu
zaidi nchini Uturuki na kuimarisha
zaidi shirika letu.
Kama Green crescent, hatua nyingine
tunazochukua ni pamoja na kushiriki
mikutano, makongamano na warsha
kuhusu utumiaji madawa ya kulevya
iliyoitishwa na mamlaka za sifa
duniani kote, na kuwakilisha nchi
ya Uturuki vyema. Aidha, tunaleta
pamoja mamlaka za kimataifa kutoka
duniani kote kwa ajili ya mikutano,
kwa mfano Mkutano wa pili wa
kimataifa juu ya Sera ya Madawa ya
kulevya na Afya ya Umma, uliokuwa
mwezi wa novemba 2018, na kuandaa
mashindano ya kuhamasisha watu
kwa mfano Mashindano ya Vigorogosi
ya kimataifa ya Green Crescent. Mbali
na kuwa mjumbe kwenye Bodi ya
Ulaya dhidi ya Madawa ya Kulevya
(EURAD), shirika la Green Crescent pia
ni mwanachama wa vyama vingine
sifika, kama Muungano wa Ulaya wa
Sera za Pombe (EUROCARE); Chama
cha Kimataifa cha Uchunguzi wa Sera
za Madawa ya Kulevya (ISSDP); Kamati
ya Vienna ya Mashirika yasiyo ya
Kiserikali, ambao ni mtandao wa Ofisi
ya Umoja wa Mataifa kuhusu Madawa
ya Kulevya na Jinai (UNODC); na
Ushirikiano wa Kimataifa wa Sera za
Madawa ya kulevya (IDPC). Kila mwaka
tunahudhuria na kutoa hotuba kwenye
mikutano ya Kamati ya Madawa ya
Kulevya iliyotayarishwa na Ofisi ya
Umoja wa Mataifa juu ya Madawa ya
kulevya na Jinai (UNODC)
Tukiwa na lengo la kufikisha kazi na
huduma zetu kwa makundi yenye
mahitaji, shirika la green Crescent
linajitahidi kuzidi kushirikiana na
wadau wenye sifa, kupanua mtandao
wake wa kutoa huduma za bure kwa
jamii, na kuimarisha nafasi yake kama
mtaalamu na kiongozi wa mashirika
mengine katika ngazi za kitaifa na
kimataifa.
Ungependa kutuma ujumbe gani
kwa dunia nzima na jamii yetu
kuhusu vita dhidi ya utumiaji
madawa ya kulevya?
Katika jamii yoyote unayotoka, kulewa
ni shida ambayo inafaa kuepukikana,
pamoja na kukabiliwa vikali. Hata
hivyo, tunaweza kufaulu kupambana
nayo kama tutakubali kwamba kulewa
ni balaa ambayo tunaishi nayo tayari,
na inayoweza kuathiri kila mmoja
wetu. La kutatanisha ni kwamba balaa
hii
iliyotuzingira
haijatambuliwa
kijamii, jambo ambalo linaleta kikwazo
katika vita vya kupambana nayo. Kwa
hiyo, inatubidi kutafuta masuluhisho
badala ya kubeza shida hii. Ili kuikabili
shida hii, ambayo tayari imetanda
dunia nzima, tunahitaji ushirikiano
na miradi Zaidi katika Nyanja za
uzuiaji, usuluhishaji na matibabu kwa
waathiriwa. Ni muhimu sana kwamba
sehemu zote za jamii zijitahidi kutoa
huduma za afya zilizo bora, ambalo
ni lengo la kila mdau duniani kote.
Tutaendelea kujitahidi kadri ya uwezo
wetu ili kutimiza lengo hili katika
ngazi ya kitaifa na ya kimataifa.
Tumechukuwa hatua kubwa
kutangaza vita vyetu dhidi
ya utumiaji madawa ya
kulevya nje ya nchi yetu
pamoja na kubeba jukumu
la kuwa kiongozi wa vita
hivi duniani. Hatua muhimu
zaidi katika shughuli hizi
ilikuwa kuunganisha
Mashina ya kitaifa ya Green
Crescent ili kusambaza vita
vyetu dhidi ya kulewa kwa
nchi mbalimbali duniani
kote chini ya mwavuli wa
shirika moja.
6