

Shirika la Green Crescent limefanya
miradi ambayo imekuwa mfano wa
kuiga duniani. Elezea zaidi miradi
na shughuli za Green Crescent,
kama shirika ambalo ni imara na
lililodumu.
Tangu kuanzishwa kwake, Green
Crescent
limekuwa
uwanjani
katika ngazi ya kitaifa na kimataifa
likipambana dhidi ya kulewa pombe,
madawa, sigara na teknolojia. Shirika
hili linapiga vita dhidi ya aina zote za
kulewa zenye madhara kwa binadamu,
sio tu kwa aina mbili za sigara na
madawa, kwani aina za vilevyo huwa
zinabadilika sana. Vita ambavyo
shirika hili linapigana dhidi ya aina
zote za kulewa ndivyo vinalitofautisha
na mashirika mengine yasiyo ya
kiserikali duniani kote. Shirika la green
crescent linaandaa na kutekeleza
shughuli na miradi yake yote kwa
kuzingatia ulingano unaoweza kuwepo
baina ya vilevyo mbalimbali.
Katika mtazamo wa kihistoria, shirika
la Green Crescent limetanguliza
shughuli za kuzuia na kutoa suluhisho
katika harakati zake dhidi ya kulewa.
Mkabala bora zaidi wa kupambana
na kulewa ni kuzingatia shughuli za
kuzuia vitendo vya kulewa vyenyewe.
Katika
mkutadha
huu,
kwanza
tulianzisha Mpango wa Kuzuia Kulewa
nchini Uturuki, ambao umetajwa na
shirika la Umoja wa Mataifa kuwa ni
mfano wa kuiga kwa nchi nyinginezo.
Katika jukwaa hili la ushirikiano
wetu na wizara ya Elimu ya Taifa,
tumehamasisha wanafunzi wapatao
milioni 10 na watu wazima milioni
mbili kila mwaka. Kisha,tukiwa na
lengo la kutabiri makundi yaliyo
hatarini na kuyakimbilia kabla kulewa
hakujatokea,
tulianzisha
Mpango
wa Kusuluhisha Kulewa Shuleni kwa
wanafunzi wa shule za sekondari,
kwani hatari ya kulewa ipo juu Zaidi
miongoni mwa rika hii. Kwa upande
mwingine, kupitia Mpango wa Stadi wa
Maisha, tumehimiza vijana na watoto
kuwa na msimamo imara maishani
mwao wakati wakikabili hali ngumu,
kukataa kushiriki miendendo isiyofaa,
kudhibiti hasira na kuanza kujifunza
au kushiriki stadi mpya. Isitoshe,
tumejitahidi kuimarisha mapambano
yetu kupitia miradi kama “Chama
Changu: Green Crescent”, kampeni,
machapisho, warsha za kitaifa na za
kimataifa, na makongomano.
Ili kupiga kijinji harakati zetu
za kukimbilia na kuzuia kulewa,
tulichukuwa hatua za kwanza mwaka
2013 katika uwanja wa kukarabati
waathiriwa
kupitia
shughuli
za
kukaribisha wote katika mipango
ya kukarabati katika sharia zetu.
Tulianzisha “Vituo vya Ushauri vya
Green Crescent”, ambapo tunatoa
huduma za ushauri dhidi ya kulewa
pombe na madawa pamoja na wana-
familia wao bila malipo. Kisha tulianza
kujenga “Kituo cha Ukarabati cha
green crescent” kilichoanzishwa kwa
kuzingatia utamatuni wa Uturuki, na
kilitoa matibabu, huduma za kutunza
wagonjwa waliolazwa hospitalini na
kutoa ajira kwa wagonjwa, ambapo
pia
tulishughulikia
wana-familia,
kama viambajengo vya jamii. Kazi zetu
zinazidi kulenga uimarishaji wa mradi
wa Kituo cha Ukarabati cha Green
Crescent.
Tukizingatia miradi hii yote, tunaweza
kusema kwa uhakika kwamba itakuwa
miradi sifika katika ngazi ya kimataifa
na itaweza kuwa mifano bora ya kuiga
kwa nchi nyinginezo.
Tunaamini kwamba njia tu
ya kulea vizazi vyenye afya
na uzima tunavyotamani ni
kuhakikisha kwamba kila
mtu, kutoka umri wa miaka
7-77 anashirikishwa kwenye
vita hivi.
Makao makuu ya Green Crescent
5