

Shirika la Green Crescent lilianzisha idara inayoshughulikia kazi
na miradi ya kimataifa ya kukabili ulevi, inayoitwa Shirikisho
la Kimataifa la Green Crescent, na hukumbana na ulevi
ulimwenguni kote kupitia mashina ya kitaifa ya Green Crescent.
Osman Baturhan Dursun, ambaye ni Katibu Mkuu wa Green
Crescent, alizungumza nasi kuhusu shirikisho la Kimataifa la
Green Crescent, na namna safari ilivyokuwa hadi sasa katika vita
dhidi ya ulevi.
Tafadhali elezea mwanzo wa
Shirikisho la Kimataifa la Green
Crescent pamoja na malengo yake.
Shirikisho hili lilianzishwa tarehe 7
Novemba 2017 chini ya uongozi wa
shina la Green Crescent la Uturuki, kwa
lengo la kujishirikisha zaidi kwenye
miradi ya kimataifa katika vita dhidi
ya ulevi, pamoja na kuwa mstari wa
mbele katika kupinga sigara, madawa
ya kulevya, kulewa teknolojia na
kulewa Kamari, na pia kuinua uwezo
wa mashina ya kitaifa na kuratibu
mtandao wa mashina hayo. Katika
muhula wake kama Waziri mkuu,
Bwana Recep Tayyip Erdoğan, Rais wa
Jamhuri ya Uturuki, alitunga shabaha
la mstakabali la Shirikiso hili. Misingi
ya Shirikisho hili ina mizizi yake katika
shina la Green Crescent la Uturuki,
shina la miaka mingi zaidi na lililo
imara zaidi duniani katika vita dhidi ya
ulevi. Lengo lake ni kupasha mashina
ya nchi nyinginezo uzoefu wake wa
miaka mingi katika kupigana na ulevi.
Hivi leo, zaidi ya mashina ya kitaifa
70 yanatekelza shughuli zake chini ya
uangalizi wa Shirikisho hili.
Shina la Uturuki ndilo shirika tu
lisilo la kiserikali duniani ambalo
limechukuwa mkabala wa pamoja wa
kupigana na ulevi. Shirika la Green
Crescent ambalo lilianzisha mwaka
wa 1920 halina kifani duniani, na
kwa hiyo ingawa kuna mashirika
mengine yanayopigana na sigara,
pombe, madawa ya kulevya na ulevi
wa teknolojia na Kamari, hakuna
jingine isipokuwa Green Crescent la
Uturuki ambalo linatumia mkabala
wa kuleta pamoja mashina yake. Hivi
vita vya ulimwengu dhidi ya ulevi
vimetuonyesha kwamba kupigana
dhidi ya sigara au pombe haitoshi
katika vita dhidi ya ulevi, na inatubidi
kutumia mkabala wa pamoja na
kuanzisha vita dhidi ya aina zote za
ulevi wakati mmoja. Tatizo la ulevi
katika nchi moja huweka nchi nyingine
hatarini, na ndiyo sababu tunahitaji
kuchukua hatua katika ngazi ya dunia
kupigana na aina zote za ulevi. Lazima
dunia nzima iwe na ubia katika vita
hivi, na kushughulika kwa nia ya udugu
na watu wote. Hii ndiyo nia kuu katika
uanzishaji wa Shirikisho hili pamoja na
mashina ya kitaifa ya Green Crescent.
Lengo la Shirikisho ni kuratibu kazi za
mashina ya kitaifa ya Green Crescent
katika nchi mbalimbali duniani kote,
kuzipasha uzoefu na ujuzi wake, na
kupigana na ulevi ulimwenguni kote
kwa kutumia mkabala wa pamoja kwa
misingi ya kisayanzi.
Picha ni za: Semih Akbay
OSMAN BATURHAN DURSUN,,
KATIBU MKUU WA SHIRIKA LA GREEN CRESCENT:
“SHIRIKA LA
GREEN CRESCENT
LIMEPELEKA VITA DHIDI
YA ULEVI KWENYE
JUKWAA LA DUNIA”
Tangu kufuzu shahada ya sharia kutoka Chuo
Kikuu cha Marmara, Ndaki ya Sheria mwaka
2001, Osman Baturhan Dursun amekuwa
akifanya kazi zake kama mwanasheria huru, na
alianzisha na kusimamia mashirika mbalimbali
yasiyo ya kiserikali. Hivi sasa yeye ni Katibu
Mkuu wa shina la Green crescent la Uturuki na
Shirikisho la Kimataifa la Green Crescent, akiwa
na majukumu mbalimbali katika mashirika
mengi ya kitaifa na ya kimataifa.
OSMAN BATURHAN DURSUN NI NANI?
10