Background Image
Previous Page  19 / 68 Next Page
Information
Show Menu
Previous Page 19 / 68 Next Page
Page Background

hizo mbili za ufanisi zilizofanywa

kote nchini Uturuki mnamo 2016 na

2018 zilionesha ufanisi wa TBM katika

kukuza ujuzi na katika kufikisha

habari.

Barua na brosha zote zilizotayarishwa

kwa TBM, ambazo maudhui yake

yanaweza kupatikana kwenye tovuti

tbm.org.tr, zilitumwa kwa wale ambao

walitoa maombi kupitia tovuti hiyo

bila malipo. Takriban brosha milioni

8 na mabango 100,000 yalisambazwa

kila mwaka.

Waratibu wa TBM watoa habari

kwa watu wengine kuhusu

waliyopitia

Ili kuboresha maarifa ya waratibu

wa TBM katika uwanja wa ulevi

wa madawa, na kuwatia hamasa

na

kushughulikia

changamoto

zinazowakabili uwanjani, Mpango wa

Kuimarisha Uwezo wa Waratibu wa

TBMulitekelezwa,GreenCrescentikiwa

ndiyomwenyeji wa mpango huo. Ndani

ya mfumo wa mpango uliotekelezwa

mnamo Juni 2019, wanajumuiya na

wakufunzi wa Kamati ya Kisayansi

pamoja na wataalam kutoka Kituo

cha Green Crescent cha Mafunzo

na Ushauri (YEDAM) waliwasilisha

na kutoa kozi za mafunzo. Mbali

na mafunzo yaliyotolewa, shughuli

za kuzidisha motisha ziliongezwa

kwenye programu na changamoto

zinazowakabili uwanjani zikajadiliwa.

Takriban maskauti 60,000

wapokea mafunzo ya TBM

Kwenye kambi za vijana zilizoandaliwa

na Shirikisho la Ukaguzi na Uongozaji

la Uturuki, Green Crescent imetoa

mafunzo ya TBM kwa wanajumuiya

takriban 60,000 wa mashirika hadi

leo, kwa lengo la kuwahami dhidi ya

ulevi wa madawa. Tangu 2013 watu

wa Green Crescent kama 80 wenye

kujitolea

wamekuwa

wakiwapa

watoto na vijana fursa mbalimbali,

wakipanga shughuli zinazowaruhusu

kufurahia muda wao wa kupumzika na

kupata stadi tofauti za maisha, huku

wakiepuka aina yoyote ya ulevi wa

madawa.

TBM kupanua shughuli zake pia

mpaka kwenye sekta binafsi

Green Crescent imepanua mafunzo

yake ya TBM pia kwenye sekta binafsi

ikifuata sekta ya umma. Mpango wa

TBMwa Green Crescent umesambazwa

kwa zaidi ya wafanyakazi 3,000 katika

ofisi kuu ya TYH katika Tekstil huko

Istanbul, na katika mikoa mingine

nchini Uturuki. Chini ya mpango

huo, mafunzo ya TBM yalitolewa

na wakufunzi wataalam wa Green

Crescent kuwasaidia watu kuanza

tabia ya kuishi maisha yenye afya.

Green Crescent inajibu maombi ya

mafunzo ya TBM yaliyopokelewa

kutoka kwa taasisi na mashirika.

17