

Vilevile, mipaka imeondolewa, intaneti
imesambaa duniani kote na maendeleo
mengine kama hayo pia yametokea, na
hatimaye, vifaa ya kulevya vimewza
kupatikana kwa urahisi sana na kwa
njia rahisi sana. Bila hiari, tatizo la
ulevi limekuwa tatizo kubwa zaidi kwa
haraka sana. Kwa mtazamo huu, kila
asasi na shirika, sanasana mashirika
yasiyo ya kiserikali, yana jukumu katika
vita dhidi ya ulevi. Iwapo mashirika
yasiyo ya kiserikali yatafaulu, serikali
lazima ziyakubali na kuyapa usaidizi
katika harakati zake.
Umetaja kwamba kuna majukumu
makubwa ambayo lazima mashirika
yasiyo ya kiserikali yachukuwe
katika vita dhidi ya ulevi. Tafadhali
zungumzia Green Crescent, kama
mojawapo ya mashirika , na
twambie juu ya mkabala wake dhidi
ya ulevi.
Shirika la Green Crescent limedumu
kwa miaka 100, ni shirika lililoimarika
sana katika mapambano dhidi ya ulevi.
Wakati mwingine, ukongwe wa shirika
unaweza kulifanya likwame, na kuwa na
idara zisizo na kasi na ambazo haziwezi
kustahimili kasi ya mabadiliko ya siku
hizi. Licha ya kudumu kwa miaka 100,
shirika la Green Crescent limekwepa
mtego huu, na limetekeleza miradi
yenye uvumbuzi mkubwa na ambayo
imekuwa mfano wa kuiga katika
ngazi ya taifa na kimataifa katika vita
dhidi ya ulevi duniani kote. Shirika
hili lilikuwa la kwanza kuorodhesha
ulevi wa teknolojia kama mojawapo ya
ulevi wa hatari sana wa kizazi hiki, na
kufanya utafiti katika uwanja huo.
Hivi leo, tunajishughulisha na aina tano
kuu za ulevi—pombe, sigara, teknolojia
na kamari. Sisi kama Green Crescent,
mkabala wetu katika kukabili ulevi
ni ufuatao: mara tu mtu anapoanza
kuelemewa na ulevi, mchakato husika
wa kumtibu na kumkarabati huwa ghali
sana kwa jamii, mkiwemo gharama za
kifedha, kihisia na kimaadili. Katika
taaluma ya saikolojia, huwa tunarejelea
dhana ya “miaka potezwa”, kumanisha
kile kipindi ambacho mtu hakuwa
na mchango wowote kwa sababu ya
ulevi. Huo ni muda ambao mtu huyu
angaliutumia kujiendeleza, kutumia
vipawa vyake na kupata tajriba,
lakini huo muda wote ulipotezwa mtu
akishiriki ulevi. La mihumu sana ni
kwamba walevi hupoteza matumaini,
heshima na furaha juu ya maisha yao
na ujao wao. Sisi kama Green Crescent
tunajitahidi kuona kwamba hakuna
anayeshindwa kuona thamani ya
utu kwa sababu ya ulevi. Bila shaka
tunafahamu kwamba ulevi huwa na
athari za aina mbalimbali zisizoweza
kupuuzwa
katika
jamii,
ambazo
husababisha madhara ya kiuchumi,
matatizo ya kijamii na makosa ya
jinai. Hata hivyo, huwa tunazingatia
athari hizi zote kama miaka, furaha
na matumaini ambayo mtu hutu
alipoteza. Matatizo hayo hayaathiri tu
mtu aliyeelemewa na ulevi, lakini pia
huathiri binadamu kwa jumla. Kwa
hiyo, ingawa huwa tunatazamia hasa
utafiti wa kisayansi na takwimu zaulevi,
data ya msingi kwetu si takwimu, bali
ni idadi ya watu tunaofaulu kunusuru.
Kwa sababu hiyo, harakati zetu zote
zinalenga kuhakikisha kwamba watu
kamwe wasinaswe na ulevi, na kwamba
wanaweza kujilinda dhidi ya mienendo
ambayo inasababisha ulevi.
Ni mikakati gani ya kukinga na
kukarabati walevi ambayo shirika
la Green Crescent limetekeleza hadi
sasa?
Sisi kama Green Crescent tunatekeleza
Mpango wa Mafunzo ya kupambana
na Ulevi wa Uturuki, ulioandaliwa
kutokana na jitihada kubwa za
wanasayansi wetu ambao wametumia
muda mrefu kutayarisha kazi hii. Kwa
kushirikiana na Wizara ya Elimu ya
Taifa kila mwaka tunatoa habari za
kweli kuhusu ulevi kwa watoto na
vijana wapatao miliyoni 10 wanaosoma
shule za msingi, sekondari ya nchini
na ya juu katika mikoa yote 81 ya
nchi Uturuki. Tunaendelea kutoa
na kusambaza habari nyepesi lakini
muhimu kuhusu ulevi kwa watu wengi
kadri tunavyoweza, kupitia ushirikiano
wetu na asasi rasmi kama vile Ofisi ya
Rais naMasuala yaDini, Wizara ya ulinzi
wa Taifa, serikali za mitaa na mashirika
mbalimbali yasiyo ya kiserikali.
Aidha, kamaGreenCrescent tumeandaa
Mpango wa Shule wa Kuitikia Ulevi
wa kuwasaidia vijana ambao tayari
wanatumia madawa ya kulevya lakini
hawajaelemewa na ulevi. Kupitia
mpango huu, tunalenga kulinda vijana
walio hatarini, na kuwasaidia kurudi
kwa mwenendo wa maisha ambao
wanaweza kuishi kwa uhuru kabisa.
Mbali na kutoa habari kwa wale
wasioelemewa na ulevi na kutekeleza
mpango wa kusaidia wale ambao
tayari wameanza kuelemewa na ulevi,
tumeanzisha mpango mwingine wa
kuwasaidia watoto na vijana wetu
kupata stadi muhimu ili kuhakikisha
kwamba
wanaweza
kuchukua
msimamo imara na uchaguzi wenye
busara wanapokabiliwa na ulevi,
tukifahamu kwamba stadi hizo ni
baadhi ya zile za muhimu zaidi katika
vita dhidi ya ulevi. Tumeandaa mpango
wa stadi za maisha wa Green Crescent
na tutaanza kuutekeleza hivi karibu.
Mbali na machapisho yanayolenga
watoto na vijana moja kwa moja,
tunatoa
pia
machapisho
mengi
yanayolenga
kuwahamasisha
wanajamii kwa jumla kuhusu ulevi,
na kuelekeza jamii yetu kung’ang’ania
maisha yenye afya. Miongoni mwa
machapisho muhimu zaidi katika
uwanja huu ni Jarida la Green Crescent,
ambalo tumekuwa tukichapisha kila
Sisi, kama shirika la Green Crescent, tunajitahidi kuhakikisha
hakuna mtu anayepoteza heshima ya utu katika mtego wa ulevi.
19