

Gilberto Gerra, MD, Mkuu wa Idara ya Kuzuia Madawa ya kulevya na Afya
chini ya Idara ya Utendaji ya UNODC, ambaye ni mwanasayansi mashuhuri
katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya anasema kwamba;
“UNODC inaangazia kwamba Green Crescent itafanya kazi kubwa ya
kiuongozi imara katika kiwango cha kimataifa katika miaka ijayo.”
Je, Unaweza kutwambia msimamo
wa dunia kuhusu utumiaji wa
madawa ya Kulevya?
Uraibu wa madawa ya kulevya
hutambuliwa kama shida tata ya
kiaafya iliyo na njia maalum ugonjwa
unavyokua
yaani
pathogenesis
inayoweza kuepukwa na kutibibika.
Mifumo ya zamani ambayo kwayo
utumiaji wa madawa ya kulevya
uliangaliwa kama uhalifu, upungufu
wa maadili, kama zoezi la burudani au
hali ya jamii, vimepitwa na wakati.
Kwa Kufuatia Kikao Maalum cha
Mkutano Mkuu wa Umoja wa
Mataifa kuhusu Tatizo la Madawa ya
Kulevya Duniani mnamo 2016, nchi
wanachama zilitambua umuhimu wa
kufuata mtazamo wa kiafya kuhusu
utumiaji wa madawa ya kulevya na
shida za utumiaji wa madawa ya
kulevya, wakajitolea “kukuza afya,
ustawi na afya njema ya watu wote,
familia na jamii kwa ujumla, na
kuwezesha maisha yenye afya njema
kupitia mipango madhubuti, kamili,
ya kisayansi ya kupunguza mahitaji
ya madawa ya kulevya katika ngazi
zote ... “(Hati ya Matokeo ya UNGASS,
uk. 4). Hii ni ishara ya daraja ambalo
limejengwa kati ya sayansi, sera
ya madawa ya kulevya na utendaji,
vinavyosababisha huduma kamili kwa
wagonjwa na wateja kote duniani
Je! Ni nini kinachofanywa kulinda
afya ya umma ya ulimwengu, na ni
nini kimepangwa kwa siku zijazo?
Katika kipindi cha miaka 12 iliyopita,
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya
madawa ya kulevya na Jinai (UNODC)
imefanya kazi katika nchi zaidi ya
50 ili kuelekeza zaidi uongezekaji wa
bingwa na wataalamu katika uwanja
wa tiba ya madawa ya kulevya na
imejaribu mipango ya kuzuia utumiaji
wa madawa ya kulevya kwa kuegemea
ushahidi mkali kwa shule na familia.
Hili limefanywa kupitia utengenezaji
wa hati za kuonyesha mazoezi,
kama vile Viwango vya Kimataifa
vya Kuzuia Matumizi ya madawa ya
kulevya vya Kimataifa vya Tiba ya
Matatizo ya Matumizi ya madawa ya
kulevya zilizofanywa kwa kushirikiana
na Shirika la Afya Duniani. Kwa
kuongezea, UNODC imeongeza uwezo
wa watunga sera na watendaji kupitia
mafunzo mengi na mipango ya
uongozi.
Pamoja na mabadiliko ya mtazamo
wa kiafya wa dunia, nchi Wanachama
zimeanza kuhama kutoka mtazamo
wa kuweka vikwazo na kuadhibu na
kuanza kutumia mtazamo wa utunzaji
wa afya na kukubaliwa kwa waraibu na
jamii, na UNODC imewezesha mbinu
inayoangazia mwendelezo wa utunzaji
wenye mwelekeo wa kuponnya, kutoa
mahitaji maalum ya mtu aliyeathiriwa
katika nyakati tofauti za ugonjwa.
Nchi wanachama zinapaswa kuhama
kutoka kwa hatua zilizofanywa kwa
kutengwa na kuchukua mitazamo
unaounganisha njia za kisaikolojia
ya jamii na kifamasia, ikijumuisha
Mahojiano na: Fatıma Aydın
GILBERTO GERRA, MD:
“GREEN CRESCENT
YAENDELEA KUWA
KIONGOZI MKUBWA
WA DUNIA”
Gilberto Gerra, MD, alizaliwa huko
Parma, nchini Italia. Alimaliza masomo
yake ya chuo kikuu katika Shule ya
Tiba ya Chuo Kikuu cha Parma. Hivi
sasa anafanya kazi kama mtaalamu
wa magonjwa ya watu wazima na
daktari wa mfumo wa tezi yaani
endocrinologist. Wakati wa kazi yake
ya kitaalam amefundisha katika vyuo
vikuu vingi nchini Italia katika uwanja
wa nyurodokrinolojia na maduka
yanayouza dawa bila kufanya vipimo
vya kimaabara . Alifanya kazi katika
Kituo cha Matibabu ya Madawa ya
Kulevya huko Parma kati ya mwaka
1982 na 2003, akafanya kazi kama
Mkurugenzi wa taasisi hiyo kutoka
1995 hadi 2003, na katika kipindi
hicho hicho alifanya kazi pia kama
Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa
Uraibu wa madawa ya kulevya huko
Parma.
Kisha akaendelea kuwa Mkurugenzi
wa Uchunguzi wa Kitaifa wa madawa
ya kulevya wa katika Ofisi ya Waziri
Mkuu, Roma, Italia, na alikuwa
Mwanachama wa Bodi ya Kimataifa
ya kudhibiti madawa ya kulevya ya
Nakotiki (INCB) kwenye Umoja wa
Mataifa, huko Vienna. Tangu 2007,
amefanya kazi kamaMkuu wa Tawi la
Kuzuia madawa ya kulevya na Afya,
Idara ya Operesheni, Ofisi ya Umoja
wa Mataifa ya madawa ya Kulevya na
uhalifu huko Vienna.
KUHUSU GILBERTO GERRA, MD
24