Background Image
Previous Page  27 / 68 Next Page
Information
Show Menu
Previous Page 27 / 68 Next Page
Page Background

mikakati ya kibinafsi na ile ya

kutofautisha. Kwa kuunga mkono

mabadiliko haya, UNODC inahimiza

hatua madhubuti katika kila hatua

ya mwendelezo wa utunzaji, ikiwemo

utoaji wa msaada wa kiufundi kwa

nchi wanachama katika maeneo

yanayohitaji uzuizi mkali, kusambaza

kitabu kinachoonyesha vitendo bora,

na kutoa njia mbadala za kuwafunga

gerezani na kuadhibu watu walio na

shida ya uraibuwamadawa ya kulevya.

Je! Ni nini jukumu la asasi za kiraia

kuhusu dawa za kulevya?

Asasi za Kiraia zinaendelea kutekeleza

majukumu muhimu sana katika kutoa

huduma za kupunguza za mahitaji

ya madawa ya kulevya duniani.

UNODC inashirikiana kwa pamoja

na Kamati ya mashirika yasiyo ya

Kiserikali ya Vienna na kamati ya

mashirika yasiyo ya kiserikali kuhusu

madawa ili kuhakikisha kuwa wale

walioathiriwa wana sauti katika ngazi

zote za mchakato wa kutengeneza

sera . Katika kiwango cha kimataifa

na cha kitaifa, mashirika yasiyo ya

kiserikali

huongeza

mawasiliano,

ushirikiano na kubadilishana kati

ya mashirika ya Umoja wa Mataifa

na

nchi

wanachama.

Mitandao

yenye nguvu inapatikana katika

mazingira ya asasi za kiraia ambayo

inakuza uhamasishaji kuongezeka na

ambayo inasaidia utetezi muhimu,

kuwezesha uwakilishi wa idadi ya watu

walioathirika.

Mapenzi makali na kujitolea kwa

dhati ndio misingi ya asasi za kiraia.

Zinatumika kama msingi wa kujengea

njia ya afya ya umma ambayo

inaegemea katika ulinzi wa haki za

binadamu za wagonjwa; utoaji wa

huduma kwa wakati unaofaa na mzuri

katika kuzuia matumizi ya madawa ya

kulevya; matibabu ya shida za utumiaji

wa madawa ya kulevya; kutibu na

urekebishaji wa waraibu wa madawa

ya kulevya; na kupunguza ubaya wa

kiafya na kijamii unaohusishwa na

utumiaji wa madawa ya kulevya,

ikiwemo pia na wale ambao hujipiga

sindano ya madawa ya kulevya.

Washirika wa asasi za kiraia kote

duniani wameunga mkono mabadiliko

hayo kwa mtazamo wa afya katika sera

ya madawa ya kulevya na wamekubali

utegemezi mkubwa kwa sayansi na

inayotegemea ushahidi.

Je! Unafikiria nini juu yamapambano

ya Green Crescent dhidi ya Uraibu

wa madawa ya Kulevya?

UNODC inajivunia kuwa mshirika wa

Green Crescent, na inapongeza kazi

nzuri inayofanywa kuzuia matumizi

ya madawa ya kulevya na tabia

zingine hatari. Green Crescent ina

mtandao wa kuvutia wa matawi 120 na

mamia ya maelfu ya wafanyakazi wa

kujitolea wanaofanya kazi kwa pamoja

kuunda mashirika huru zaidi ya 50, na

kuyaunganisha mashirika haya yote

chini ya Shirikisho kubwa la Kimataifa

la mashirika ya Green Crescent,

sawa na mwavuli. Green Crescent

pia inawakilisha Uropa ya Mashariki

na Asia ya Kati kama mwanachama

wa Kamati ya Mashirika yasiyo ya

kiserikali ya madawa ya kulevya.

Katika kiwango cha kimataifa, Green

Crescent imeanzisha hafla kadhaa na

kuchukua jukumu la uongozi katika

hafla za hali ya juu wakati wa Tume

juu ya madawa ya kulevya ya Nakotiki.

UNODC inaendelea kuwa mshirika

mwenye mkubwa wa Green Crescent,

na kuona majukumu bora zaidi ya

kwao katika kiwango cha kimataifa

katika miaka ijayo.

Katika

kiwango

cha

kawaida,

haisambazi tu huduma zinazoegemea

kwenye ushahidi mkali, lakini pia

huweka kiwango cha juu cha maadili

ya jamii, na katika kupunguza hatari

na kukuza ustahamilivu. Wanasaidia

na kuhimiza uingiliaji kati wa familia,

uingiliaji kati wa jamii na mwingilio

wa shule, na hujumuisha mfumo wa

umma wenye mitazamo kadhaa katika

uzuiaji.

Katika kiwango cha

kimataifa, Green Crescent

imeanzisha miradi kadhaa

na imechukua jukumu

kubwa katika ushiriki wake

katika hafla za hali ya juu

za Tume ya madawa ya

kulebya ya Nakotiki

25