

stadi ambazo zitawasaidia kuingia
taaluma kama vile sanaa ya kuandika
na kuchora picha, pamoja na sanaa ya
mapishi. Halafu tunawasaidia kupata
kazi tukishirikiana na Shirika la Ajira
nchini Uturuki (IŞKUR). Tunachukua
tahadhari kuwahimiza kuishi maisha
yenye afya, na kuyabadilisha maisha
hayo yawe mtindo wa maisha. Haya
yote ni mabadiliko makubwa katika
maisha ya mraibu. Mraibu anapata
stadi, anajihisi kuwa mtu wa maana
na anapata fursa ya kujielezea, hii
ikimaanisha kwambamtu huyo anaona
tena maana ya kuishi na kuanza
maisha mapya. Hasa, wanapopata kazi,
wanahisi wameunganishwa na jamii.
Kwa maneno mengine, tunarekebisha
maisha yao. Waraibu wa madawa ya
kulevya au jamaa zao wenye umri wa
miaka 16 na zaidi ambao wanataka
kupata huduma zetu au kupata
matibabu wanaweza kuwasiliana nasi.
Mnapanga kuanzisha vituo vingapi
vya Ushauri nchini Uturuki?
Tunakusudia kuanzisha Kituo cha
cha Green Crescent cha Mafunzo
na Ushauri katika majimbo yote 81
ya Uturuki, tukiweka zaidi ya kituo
kimoja katika miji mikubwa au katika
miji ambapo utumiaji wa madawa ya
kulevya na pombe umeenea zaidi. Hii
inamaanisha kuwa waraibu, jamaa
zao na mtu yeyote anayehitaji msaada
wetu ataweza kuwafikia wataalamu
wetu wa matibabu ya kisaikolojia kote
nchini kwa bure. Hivi sasa, kuna vituo
36 vya Green Crescent vya Mafunzo na
Ushauri nchini Uturuki.
Inawezekana kuanzisha Vituo vya
Green Crescent vya Ushauri katika
nchi zingine?
Kwa kweli, kila kielelezo na kila
mradi uliopangwa na Green Crescent
unalenga
kutoa
huduma
kwa
binadamu wote. Ingawa vituo vyetu
vya Green Crescent vya Mafunzo na
Ushauri vimeanzishwa kulingana na
hali yetu ya kipekee ya kitamaduni,
sifa za kijamii na watu, muundo
wake unaweza ukahamishwa na
kurekebishwa na nchi tofauti. Tuko
tayari kwa ushirikiano kimataifa na
tuko tayari kutoa uzoefu wowote na
maarifa ambavyo tumepata katika
uwanja wa urekebishaji.
Unaweza kutuambia kuhusu
Kituo cha Urekebishaji cha Green
Crescent, kama mradi mwingine
wa Green Crescent wa utoaji wa
huduma za urekebishaji?
Green Crescent inachukulia uraibu
kama
tatizo
ambalo
linahitaji
kukomeshwa, na juhudi zake zote
zinafanywa kulingana na lengo hili.
Mfano mmoja wa jitihada kama hiyo
umekuwa ni kuanzishwa kwa Kituo
cha Urekebishaji cha Green Crescent
– kielelezo cha kitaifa kilichoundwa
kulingana na tamaduni na maadili
yetu. Kituo hiki kiliundwa kulingana
na maelezo mafupi juu ya nchi yetu
kuhusu uraibu baada ya kuchambua
jitihada za nchi zaidi ya 20 na
kutembelea nchi 10 kati ya hizo. Kituo
hicho kiliundwa kama kituo chenye
msingi wa mtu binafsi, familia na
jamii, na kielelezo kinacholenga
urekebishaji
wa
mtu
binafsi
kiliundwa, kikilenga hasa mazingira
ya kifamilia na kijamii. Mojawapo ya
sifa za vituo vyetu inayovitofautisha
zaidi na vituo vingine katika kutoa
matibabu na mafunzo ya kiufundi ni
kuhusisha familia katika mchakato.
Katika kituo chetu, mraibu anapitia
mchakato ambapo anapewa msaada
wa kisaikolojia na kijamii, na kisha
anapata stadi za kufanya kazi fulani
ya kitaalam, kuboresha mahusiano ya
kifamilia na kujenga mahusiano imara
ya kifamilia. Wakati wanapoondoka
miezi 6 baadaye, wanafanya hivyo
wakiwa na mahusiano na stadi za
kujenga
mahusiano,
pamoja
na
taaluma ambayo wanaweza kuitumia
kutoa mchango kwa jamii, na ambayo
inawaruhusu kuungana tena na jamii.
Tunaamini kuwa hii itakuwa na athari
muhimu na tofauti kwa jamii yetu.
Tukitumia kituo hiki, tunakusudia
kurekebisha sio walevi tu, bali pia
familia zao. Tunaamini kwamba kwa
kufungua kituo hiki, Uturuki itakuwa
imara zaidi katika uwanja wa uraibu
wa madawa ya kulevya katika medani
ya kitaifa na ya kimataifa.
Ni
wazi
kuwa
Green
Crescent
imechukua hatua hii kutokana na
wajibu ambao inahisi inao kwa jamii
katika uwanja wa urekebishaji, ikiwa
na uzoefu wake wa karne nzima na
utajiri wake wa maarifa. Kwa niaba ya
nchi yetu na taifa, ninatumai kwamba
itakuwa na manufaa kwa wote.
Vituo vya urekebishaji vya
Green Crescent viliundwa
kulingana na maelezo
mafupi ya nchi yetu kuhusu
uraibu baada ya kuchambua
jitihada za nchi zaidi ya 20 na
kutembelea nchi 10 kati ya
nchi hizo. Tunaamini kwamba,
kwa kufungua kituo hiki,
Uturuki itakuwa imara zaidi
katika medani ya kitaifa na ya
kimataifa.
30