

Yeşilay’dan
Bağımlılıkla
Mücadelede
Eğitim Seferberliği
Z.T alikuwa karibu kuwa
mtawaliwa mkubwa wa kucheza
kamari.
Z.T. alikuwa karibu kuwa
mwathirika mwingine wa uharibifu
unaosababishwa na kamari.
Wakati alipoomba msaada kwa
Kituo cha mafunzo na ushauri cha
Green Crescent, Z.T. alikuwa karibu
kupoteza familia yake, lakini
alichukua udhibiti wa maisha yake
na kurudisha familia yake pendwa.
“Kituo cha Mafunzo na Ushauri
cha Green Crescent kiliyaokoa
maisha yangu ya kiroho, ikiwemo
familia yangu, marafiki wangu,
mke wangu na watoto wangu,”
anasema Z.T.
Z.T, ambaye maisha yake yalikuwa
yameharibiwa na utawaliwaji wa
Kamari, pamoja na hasara kwa
rasilmali na maisha ya kiroho,
alichukua
hatua
ya
kwanza
katika kuyaokoa maisha yake na
kupambana na kutawaliwa na
kamari kwa kutuma maombi yake
kwa kituo cha mafunzo na ushauri
cha Green Crescent. Z.T., ambaye
hakuichukua kamari kama tatizo
maishani mwake alisema kwamba,
“Niliponea chupuchupu kupoteza
Wazazi wangu, marafiki, mke na
watoto . Hapo nikaona vile uraibu
ulikuwa umeyaponza maisha yangu,
“Niliishi maisha ya Mishughuliko”
Mtawaliwa wa kamari Z.T. alielezea
hali yake kabla ya kutoa maombi kwa
kituo cha Mafunzo na ushauri cha
Green Crescent kitoacho huduma
za bure za tiba ya kisaikolojia
kwa watawaliwa/waraibu pamoja
na jamaa zao: “Kazini, nilikuwa
nikimaliza shughuli zangu zote
haraka na kuanza kucheza kamari
hadi mwisho wa siku hiyo. Mke
wangu aliponipigia simu baada
ya muda wa kazi kumalizika,
nilikuwa
nikimwambia
kwamba
bado nilikuwa na kazi za kufanya na
hivyo nilichelewa kurudi nyumbani.
Nilicheza kamari mpaka mke wangu
na watu waliokuwa karibu na mimi
kugundua hali yangu. Baada ya
muda, nilianza kupata hasara na
kwa kujaribu kulipia hasara, nilipata
hasara zaidi. Kila nilipocheza kamari
nilijiambia kwamba, hii ingekuwa
mara yangu ya mwisho lakini
sikuacha kucheza kamari. Ilikuwa ni
kana kwamba nilikuwa kwenye pingu
za kamari. Nilipoendelea kucheza
kamari, deni langu liliongezeka.
Nilikuwa na deni na kila mtu
aliyekuwa karibu na mimi na siku
moja, rafiki yangi mmoja alikuja
kwangu kudai pesa zake. Uso wa
mke wangu ulionyesha masikitiko na
mimi nilikuwa nimekata tamaa. Mke
wangu aliniuliza nimwambie shida
niliyokuwa nayo nikamwambia kila
kitu ila tu ukubwa wa madeni yangu.
Niliendelea na zoea langu nikaingia
mahali ambapo ilikuwa vigumu
kutoka, nikawa mlaghai daima,
nikaendelea kucheza kamari ili
nilipie hasara na kupata hasara tena.
“Niliyaokoa tena mapenzi ya
familia yangu ”
Z.T. aligundua jinsi tabia yake
kucheza kamari ilikuwa mbaya
wakati alipoanza kuipoteza familia
yake na wapendwa wake, mmoja
baada ya mwingine. “Uchezaji
wangu wa Kamari ulinipelekea
kufanya makosa”, alisema Z.T.,
akielezea anayoyapitia maishani
mwake: “Nilianza kupata matatizo
kazini. Marafiki zangu walikuwa
wakiniacha peke yangu kwa sababu
ya madeni niliyokuwa nayo. Nilikuwa
nikiwakatisha tamaa familia yangu,
haswa mke wangu mpendwa na
kuwafanya wakose furaha. “Akisema
kwamba alihisi kana kwamba kamari
ilikuwa imemfanya mfungwa, Z.T.
alisema kwamba kuita Kituo cha
Mafunzo na Ushauri cha Green
Crescent kumempa nafasi ya kuanza
maisha upya.
“NILIPATA TENA MAPENZI YA WAPENZI
WANGU; ASANTE GREEN CRESCENT”
34