

“GREEN CRESCENT LIMEKUWA JAMBO
KUU KWA UOKOAJI WA MAISHA YANGU ”
Sasa M.T. na familia yake wanayo maisha
mazuri na ya furahawakati ujao; shukrani
kwa Kituo cha Mafunzo na ushauri cha
Green Crescent ambacho kilikuwa hatua
ya kwamba katika harakati zake za
kujiondoa kutoka minyororo na athari
za ulevi wa pombe aliouingia alipokuwa
mdogo sana. Kama waathiriwa wengi
wa ulevi, M.T mwenye umri wa miaka 58,
hakuuona ulevi wa pombe kama shida
maishani mwake. Lakini, ni mke wake
na watoto ambao walisumbuliwa na M.T.
kunywa pombe na harakati za mwanzoni
za kumwokoa M.T. kutokana na pombe
zilifanywa nao yaani mke na watoto
wake. M.T. alikunywa pombe kuanzia
miaka yake ya ujana hadi miaka 58, lakini
aliweza kubadilisha na kuiacha tabia ya
ulevi kwa usaidizi wa Kituo cha Mafunzo
ua ushauri cha Green Crescent.
Msaada unaosababisha uokoaji
Familia ya M.T. iliyompenda sana,
lakini ikasumbuliwa sana kuishi na
mtawaliwa/mraibu wa pombe, ilianza
safari ya kumwokoa M.T, iliyoanza na
maombi yake kwa Kituo cha Mafunzo na
Ushauri cha Green Crescent. Kwa miaka
minne, wanasaikolojia wa Kituo cha
Mafunzo na Ushauri cha Green Crescent
wafanya mahojiano na mke wake
M.T. na watoto wake watatu. Baada ya
kutambua kwamba familia yake ilikuwa
imebadilika, M.T. aliuliza ni wapi na
kutoka kwa nani familia yake walikuwa
wakipokea msaada, jambo lililompelekea
kutembelea Kituo cha Mafunzo na
Ushauri cha Green Crescent kuona
kinachoendelea. M.T. alivutiwa sana na
upendo na utunzaji aliopewa na familia
yake na wanasaikolojia wa Kituo cha
Mafunzo na Ushauri ya Kijani cha Green
Crescent. Katika mahojiano yake ya
kwanza, M.T. alisema kwamba hakuhitaji
matibabu wala hakutaka kulazwa
hospitalini. Anaendelea kuzungumza juu
ya hatua iliyofuata katika mchakato huu:
“Nilijifunza kuwa inawezekana kupokea
ushauri tu bila kupewa matibabu. Hii
ilikuwa nafasi kubwa maishani mwangu.
Nilidhani, angalau hawatajaribu kunitibu
kwa nguvu, kwa hivyo nilianza kupata
ushauri nasaha. Sikumoja, bila kuijulisha
familia yangu, nilichukua miadi kutoka
kwa Kituo cha Mafunzo na Ushauri Green
Crescent ili kuanza kupata matibabu.
Nilitaka kubadilisha maisha yangu na
hali yangu. Nilikuwa na familia iliyokuwa
ikinipigania, pamoja na wanasaikolojia
wa Kituo cha Mafunzo na Ushauri wa
Kijani cha Green Cresent”
Matibabu ambayo yalibadilisha
mtazamo wangu wa maisha.
Wanasaikolojia wa Kituo cha mafunzo
na ushairi cha Green Cresent walijibu
maswali kuhusu uraibu wa pombe
na matibabu, na baada ya kuiona
familia yake ikiendelea na mahojiano
bila kuchoka, M.T, akapata mwamko
uliompelekea kikiri kwamba alikuwa na
shida kubwa sana na pombe. M.T alianza
mchakato wa kutibiwa katika Kituo cha
Mafunzo na Ushauri cha Green Crescent
kinachotoa huduma za bure za saikolojia
kwa watu wanaotawaliwa na uraibu wa
madawa na pombe pamoja na familia
zao. Bado anapata matibabu lakini kwa
sasa anaona mafanikio makubwa na
kutazamia maisha bora wakati uajo.
M.T. ni mwathirika wa pombe ambaye maisha yake yalikuwa yameathiriwa vibaya, lakini baada ya hapo aliweza
kubadilisha maisha yake wakati tu alikuwa karibu kupoteza familia yake na rasilmali yake yote. Sasa M.T. na
familia yake wanaona maisha mazuri siku zijazo; shukrani kwa maombi yake aliyotuma kwa Kituo cha Mafunzo
na Ushauri cha Green Crescent, ambayo (maombi) yalikuwa hatua yake ya kwanza kujiondoa kutokana na athari
za pombe. Kituo cha Mafunzo na Ushauri cha Green Crescent kimekuwa “jambo muhimu kwake”, anasema M.T.
33