

Kila mwaka, watu milioni saba duniani hufariki kutokana na magonjwa
yanayojihusisha na uvutaji sigara, jambo ambalo linasababisha
uzinduzi mkubwa wa mapambano dhidi ya mazao ya tumbaku.
Prof. Dkt. Toker Ergüder, Mkurugenzi wa Mpango wa Magonjwa
yasiyoambukiza katika Afisi za Shirika la Afya Duniani nchini Uturuki
aliorodhesha umuhimu wa mapambano dhidi ya Tasnia ya Tumbaku
akisema kuwa “Tumbaku ni tathnia kubwa na yenye faida kubwa
duniani.”
Unaweza kutoa mhutasari wa
msimamo wa Dunia nzima kuhusu
Uraibu wa Tumbaku?
Utumiaji wa tumbaku unaongoza
katika
usababishaji
wa
vifo
vinavyoweza kuzuiliwa nchini Uturuki
na Dunia nzima kwa ujumla; na
sekta ya tumbaku ndiyo inayoongoza
katika usambazaji wa magonjwa ya
mlipuko na hatari yanayohusiana na
tumbaku. Sasa, kuna mbinu kadhaa
zinazofaa na tafiti kuhusu uzuiaji wa
ulevi wa tumbaku, ingawa ni muhimu
kufahamu kwamba mapambano dhidi
ya utumiaji tumbaku sio mapambano
dhidi ya wavutaji sigara. Kwa kweli,
tunajaribu kuwasaidia wavutaji sigara
kuacha uvutaji na kuwasaidia kuishi
maisha yasiyoathiriwa na uraibu wa
kuvuta sigara. Baada ya kusema hayo,
mapambano yetu makuu yako dhidi
ya kampuni za sigara na tasnia ya
tumbaku. Tunaweza kusema kwamba,
tasnia ya tumbaku ndiyo tasnia kubwa
yenye faida kubwa duniani na takwimu
zilizopo zinthibitisha dai hili. Katika
mwaka wa 2017, mauzo ya rejereja ya
sigara yalifika takribani bilioni 700 za
Dola ya Marekani na hili linamaanisha
kwamba sigara trilioni 5.4 ziliuzwa
mwaka huo. Azma kuu ya tasnia ya
tumbaku ni kufungua mlango wa
uraibu wa uvutaji sigara kwa kuingiza
watoto na vijana yaani mvuto mmoja
wa tumbaku kabla hawajabarehe.
Tasnia ya tumbaku hufanikiwa katika
kampeni na mikakati yake sambamba
na malengo yake hatari. Takribani
watu milioni 7 duniani hufariki kila
mwaka kwa sababu ya magonjwa
yanayohusiana na uvutaji sigara,
huku watu milioni 1 wakifariki kwa
kuukaribia moshi wa sigara. Matumizi
ya tumbaku ni jambo hatarishi
katika vitu 6 vinavyojulikana sana
kusababisha vifo duniani kati ya 8.
Mogonjwa yamoyo, yanayosababishwa
na mishipa ya moyo kuwa nyembamba
hali inayosababisha damu kidogo na
oksijeni kufikia misuli ya moyo na
hivyo kusababisha shinikizo la damu,
magonjwa yanayohusiana na uharibifu
wa neva zinazosafirisha oksijeni
kwenye ubongo na kusababisha
kutokuwepo kwa oksijeni ya kutosha
kwenye ubongo, maambukizo ya njia
ya chini ya kupumua, magonjwa sugu
ya mapafu, kifua kikuu na saratani
zote za mapafu husababisha vifo
vinavyojihusisha na uvutaji sigara.
Saratani ya mdomo na ya koromeo,
saratani ya umio, saratani ya tumbo
na saratani ya mapafu huchangia sana
katika vifo vinavyohusiana na uvutaji
sigara.
Idadi kubwa ya wavutaji sigara
katika nchi zilizoendelea na nchi
zinazoendelea
huongeza
vifo
vinavyohusiana na uvutaji sigara
katika nchi hizi. Kwa kweli, tukiangalia
kwa mtazamo wa dunia, tunaona
kwamba ueneaji wa uvutaji sigara
unapungua, aidha hili lisiwapotoshe
wale wanaoshiriki katika mapambano
dhidi ya uraibu huu. Ingawa viwango
vya uvutaji sigara vimepungua haswa
Mahojiano na: Fatıma Aydın
PROF.DKT.
TOKER ERGÜDER:
“TUNAHITAJI
KUPAMBANA DHIDI YA
TASNIA YA TUMBAKU”
Prof. Dkt. Toker Ergüder ni Daktari wa
Matibabu na mtaalamu wa Afya ya Jamii
ambaye anafanya kazi kama Mkurugenzi
wa Mpango wa magonjwa yasioambukiza
katika Afisi za Kimkoa za Shirika za Afya
Duniani (WHO) nchini Uturuki. Pia, Prof.
Dkt. Toker Ergüder ni mhadhiri katika
Idara ya Afya ya Jamii, Kitivo cha Tiba
Gülhane, Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba.
Yeye anatoa usaidizi wa kiufundi kwa
Wizara ya Afya, kwa mashirika yasiyo
ya Kiserikali na kwa mashirika mengine
yanayohusiana na udhibiti, na usimamizi
wa magonjwa yasiyoambukiza nchini
Uturuki na mapambano dhidi ya utumiaji
wa tumbaku. Yeye ni mwanachama wa
Kamati ya Kisayansi ya Green Crescent.
Kabla yakuchukua majukumu kadhaa
katika Shirika la Afya Duniani, alifanya
kazi katika Wizara ya Afya kati ya 2002 na
2007 na kuanzisha Idara ya kupambana na
tumbaku.
Mnamo 2003,alianza kufanya juu chini
ili nchi ya Uturuki itie sahihi Mkataba wa
Mfumo wa kudhibi tumbaku na katika
uanzishaji wa Udhibiti wa Taifa wa
Tumbaku. Mnamo 2007, Gülhane alitoa
mchango mkubwa katika kutengeza upya
sheria Na. 4207 iliyoifanya nchi ya Uturuki
kuwa eneo “lisilo na Moshi wa sigara” kwa
maagizo ya Rais Recep Tayyip Erdoğan
PROF. DKT. TOKER ERGÜDER NI NANI?
36