

Kupitia mpango wake
wa Msaada wa kifedha,
Green Crescent inasaidia
mashirika ya Kitaifa ya
Green Crescent katika
juhudi zao za kuimarisha
uwezo, ili kufanya kazi za
kisayansi, na kuchukua
jukumu muhimu katika
sera za kupambana na
ulevi katika maeneo yao.
MASHIRIKA YA KITAIFA YA GREEN
CRESCENT YASHAMIRI KUPITIA MPANGO
WA MSAADA WA FEDHA WA KIMATAIFA
G
reen
Crescent
inaendelea
kutoa msaada kwa mashirika
ya kitaifa ya Green Crescent katika
mapambano yao dhidi ya uraibu wa
madawa ya kulevya katika pembe
zote nne za dunia kupitia Mpango
wake wa Kimataifa wa Usaidizi wa
Kifedha. Mpango wa Msaada wa
kifedha wa Kimataifa wa Green
Crescent unakusudia kuhakikisha
uimarikaji wa kitaifa wa mashirika
ya Kitaifa ya Green Crescent, huku
pia ukiongeza uwezo wao, na
kushawishi sera za kupambana
na uraibu wa madawa ya kulevya
kujenga miundombinu ya utetezi.
Kuhimiza mashirika ya kitaifa ya
Green Crescent kutekeleza utetezi,
utafiti wa kisayansi na majukumu
ya kuzuia uraibu wa madawa ya
kulevya katika nchi zao, Mipango
ya Msaada wa kifedha ya Kimataifa
imekusudiwa pia kusaidiamashirika
ya Kitaifa ya Green Crescent katika
kupata
miundombinu
muhimu
ya kiufundi ambayo itawaruhusu
kufanya kazi kwa ufanisi zaidi
Mpango unaotekelezwa katika
nchi 26
Huku likijitahidi kuendelezaMpango
wake wa Kimataifa wa Usaidizi wa
Fedha wa mwaka wa 2019, Mpango
wa Msaada wa Fedha wa Kimataifa
wa Green Crescent wa mwaka 2017
sasa umetekelezwa katika nchi 26,
zikiwemo; Afghanistan, Albania,
Australia,
Azabajani,
Bosnia-
Herzegovina, Bulgaria, Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC),
Kupro, Georgia, Indonesia, Kenya,
Kosovo,
Kyrgyzstan,
Lebanon,
Makedonia, Malaysia, Montenegro,
Moroko, Niger, Nigeria, Palestina,
Serbia, Somalia, Sudan, Syria na
Uganda. Mpango wa Msaada wa
Fedha wa Kimataifa wa mwaka wa
2019 hivi sasa inaandaliwa.
Maeneo ya kazi
Shughuli
zifuatazo
zinafanywa
katika Mpango wa Msaada wa
Fedha wa Kimataifa: “Kurekebisha
maudhui ya vifaa vya kuzuia
uraibu wa madawa ya kulevya
yalivyoundwa na Green Crescent
katika nyanja za uzuiaji na utetezi
kuhusu mapambano dhidi ya uraibu
wa madawa ya kulevya kwa hali ya
kiuchumi jamii ya nchi inayohusika,
na kufanya utafiti wa nyanjani;
kuunda mitandao ya ushirikiano
wa kitaifa na wa kimataifa; na
kuboresha mwingiliano wa kikanda
kati ya mashirika yote ya Green
Crescent,
kuyaruhusu
kupata
rasilimali muhimu za kiufundi
ambazo
zitawaruhusu
kufanya
kazi vizuri; kupitia maandishi ili
kujua hatari za uraibu wa madawa
ya kulevya katika viwango vya
kikanda na kitaifa; na kutoa ripoti
ya matokeo ya utafiti baada ya tafiti
za makundi kufanywa. “
Sampuli ya miradi
•
Kuandaa mashindano ya ‘Kizazi
cha Afya bora, Maisha bora ya
kiafya ya siku zijazo” katika ngazi
ya jimbo, kimkoa au kitaifa;
•
Kurekebisha maudhui ya TBM
yaani; mpango wa Mafunzo
ya kuzuia uraibu wa madawa
ya kulevya nchini Uturuki) na
kutekeleza mpango(wa walimu wa
mafunzo/walimu/walimu wa rika);
•
Urekebishaji na utekelezaji wa
Mradi wa Green Crescent ‘Chama
Changu’;
•
Kuandaa mashindano ya video
fupi na kampeni ya mawasiliano;
•
Kuwafahamisha vijana, wazazi
na wadau wengine kuhusu hatari
za uraibu wa madawa ya kulevya
na kuandaa semina na warsha ili
kuhamasisha jamii;
•
Kuanzisha klabu/vyama vya Green
Crescent katika vyuo vikuu;
•
Kukuza shirika la Green Crescent
la kitaifa; kuihamasisha umma
kupitiamatangazonakuwahusisha
watu kama wafanyakazi wa
kujitolea, wanachama, n.k.
41