

katika nchi zilizoendelea, Bara la Ulaya
bado lina viwango vya juu zaidi vya
uvutaji sigara kati ya mikoa ya Shirika
la Afya Duniani.
Je, ni Shughuli za aina gani
zinazopangwa na kufanywa ili
kuilinda jamii na Afya ya Jamii?
Kutokana na harakati zilizoanzishwa
mwaka wa 1998, Mapatano ya mfumo
wa Shirika la Afya Duniani kuhusu
udhibiti
wa
tumbaku
yalianza
kushughulikwa mwaka wa 2005. Kwa
sababu yalikuwa mapatano ya kwanza
yamfumowaUmojawaMataifakuhusu
Afya ya Jamii, mapatano yalitiliwa
sahihi na mataifa 181. Shukrani kwa
Mkutano wa Mfumo juu ya udhibiti
wa Tumbaku, nchi nyingi zilianzisha
mipango, na mkutano huo hufanya
mapendekezo kadhaa wa kiwango
cha jamii na cha mtu binafsi. Haya
hujumlisha yafuatayo: Udhibiti wa bei
na kodi ya tumbaku ili kupunguza
mahitaji yake na kuzuia magendo;
kujilinda dhidi hatari ya moshi wa
tumbaku; kuweka katika kifurushi
na uwekaji wa utambulisho kwa
mazao ya tumbaku; kupiga marufuku
matangazo ya tumbaku; ukuzaji na
udhamini; na ufuatiliaji na tathmini
yake. Mkutano huo pia unapendekeza
mbinu za kibinafsi za kuingilia kati
kama njia ya kupunguza na kumaliza
uraibu wa tumbaku.
Je, Nini jukumu la Mashirika yasiyo
ya Kiserikali katika Mapambano
dhidi ya Uraibu wa tumbaku?
Katika mapambano dhidi ya uraibu
wa tumbaku, jukumu la Mashirika
yasiyo ya Kiserikali (NGOs) ni kama lile
la serikali, na mawakala wa serikali.
Serikali haziwezi kufaulu katika
udhibiti wa tumbaku ikiwa mashirika
yasiyo ya Kiserikali hayahusishwi.
Kwa hivyo, ni jambo la muhimu sana
serikali kushirikiana na Mashirika
yasiyo ya Kiserikali ili kuihamasisha
jamii juu ya uraibu wa tumbaku na
kupunguza sana viwango ya utumiaji
wa tumbaku.
Sisi kama Shirika la Afya Duniani,
huchukua kile tunachokiita, mfumo
wa “Uhusishaji kamili wa serikali na
uhusishaji kamili wa Umma/Jamii”
ambamo mashirika yote ya serikali
hufanya kazi kwa lengo moja wakati
mashirika yasiyo ya Kiserikali haswa
Mazingira ya kitaaluma na Kisayansi,
kwa
pamoja
vitashiriki
katika
mapambano ya udhibiti mwafaka wa
tumbaku.
Pendekezo letu ni kwamba Mfumo
wa Mapatano kuhusu udhibiti wa
tumbaku upewe umashuhuri katika
nchi zote. Vile vile tunapendekeza
uchukuaji wa hatua katika maeneo
mengi kama vile: kupandisha bei ya
sigara, kutoruhusu uvutaji sigara
ndani ya nyumba na kupiga marufuku
utangazaji na matangazo wa sigara.
Unafikiri nini kuhusu juhudi za
Green Crescent katika mapambano
yake dhidi ya uraibu?
Green Crescent limekuwa Shirika lisilo
la Kiserikali la muhimu sana katika
mapambano dhidi ya uraibu wa dawa
za kulevya na tumbaku nchini Uturuki
tangu mwaka wa 1920. Tumefanya
tafiti nyingi na Green Crescent, haswa
zile zinazohusiana na mapambano
dhidi ya tumbaku. Kwa sababu ya kuwa
na nafasi maarufu katika mapambano
dhidi ya uraibu/ulevi nchini Uturuki,
Green Crescent inachukua hatua
madhubuti kuelekea kuwa mtendaji
wa kimataifa kupitia majukumu na
miradi yake ya kimataifa. Napenda,
kuwashukuru Green Crescent kwa
msaada na jihudi zao wanazotoa.
Katika miaka ijayo, Green Crescent
watakuwa Shirika lisilo la Kiserikali
muhimu sana katika mapambano
dhidi ya tumbaku na madawa mengine
katika Umoja wa Mataifa na kwa
kiwango cha kimataifa. Watakuwa na
nguvu na rasilmali kutoa msaada wa
kiufundi na kifedha kwa wale ambao
wanahitaji kufanya kazi katika uwanja
huu katika nchi nyingi duniani.
Pendekezo letu ni kwamba
Mfumo wa Mapatano
kuhusu udhibiti wa
tumbaku upewe umashuhuri
katika nchi zote. Vile
vile tunapendekeza
uchukuaji wa hatua katika
maeneo mengi kama vile:
kupandisha bei ya sigara,
kutoruhusu uvutaji sigara
ndani ya nyumba na kupiga
marufuku utangazaji na
matangazo wa sigara.
Seyyed Mohsen Nouri Najafi - I
r
an
37