

Ikumbukwe kwamba Mpango wa Uturuki wa
Kupambana na uraibu wa madawa umetajwa
kama “Utendaji Bora” katika ripoti ya EMCDDA, Işık
alisema kwamba Green Crescent inaheshimiwa
na kutambuliwa na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali
kama “kiongozi wa maoni” yanayoshughulikia
malengo sawa na yele ya Green Crescentduniani.
Shukrani kwa shughuli za mfano wa kuigwa:
“Pamoja na uzoefu wake wa karne, Green Crescent
anasema na kutenda kama “kiongozi wa maoni”
sio tu kwenye uwanja wa kitaifa, bali pia kimataifa.
Hali yake kama shirika linalohusika na mitandao
katika nchi 52 duniani kote ambayo inashiriki
uzoefu wake na Mashirika Mengine yasiyo ya
Kiserikalini kiashiria muhimu zaidi cha kazi yake
kama kiongozi wa maoni. Kazi zetu nzuri na miradi
ya mfano imesababisha sisi kuonekana kama
kiongozi wamaoni naMashirika Yasiyo ya Kiserikali
yanazofanya kazi kwa malengo sawa ulimwenguni.
Mkutano wa leo wa Istanbul Initiative ni kiashiria
cha msimamo wetu kwenye jukwaa la Dunia. “
“Azimio ni hatua muhimu sana”
Akizungumzia kuhusu azimio hilo, , ambalo
linaelezea mikakati ya kiutendaji itakayochukuliwa
katika nchi zote zinazohusika katika mapambano
dhidi ya uraibu wa madawa ya kulevya, Işık alisema
kwamba, “Mbali na sababu za kijamii na kisaikolojia,
kuwepo watendaji wengineyapaswa kukubaliwa
kama nguvu kazi. . katika ongezekolamadawa
ya kulevya. Tatizo liko mielekeo anuai Mashirika
yasiyo ya Kiserikali yanaporudi katika nchi zao,
yanahitaji kushughulikia suala hilo katika kiwango
kinachokubalika na kiwango cha Umoja wa
Mataifa na mashirika ya kimataifa ya kiafya kama
vile; Shirika la Afya Duniani (WHO). Wanapaswa
kuzingatia mapambano haya kama jukwaa pana
ambalo wanahitaji kushirikiana mawakala wa
serikali na jeshi la polisi nchini mwao.. Azimio
la kujituma la Istanbul linajumuisha kanuni na
mapendekezo kama haya.”
“Tofauti za dawa zinaongezeka barani Ulaya”
Akirejelea Ripoti ya madawa ya kulevya na uraibu
wa madawa ya Kituo cha Ufuatiliaji wa madawa ya
kulevya za Ulaya (EMCDDA), Işık alisema kwamba
aina za dawa za kulevya huko Ulaya zimeongezeka:
“Ripoti hiyo inadokeza kuongezeka kwa utumiaji
wa aina mbili au zaidi za dawa ya kulevya (yaani,
polydrug) miongoni mwa watumizi wa dawa za
kulevya. Kuenea kwa bangi, kama dawa ya kulevya
inayotumiwazaidibaraniUlaya,ikojuuyamaratano
kulikomadawamengine ya kulevya. Hadi mwishoni
wamwaka 2018, zaidi yamadawa 730 ya kisaikolojia
yameripotiwa duniani kote, 55 kati ya madawa hayo
yamegunduliwa kwa mara ya kwanza mnamo 2018
huko barani Ulaya. Kwa bahati mbaya, Uturuki ni
nchi inayounganisha Ulaya na Mashariki ya Kati,
na kwa hivyo ni njia kuu ya biashara haramu ya
madaya ya kulevya kuna aina nyingi kutoka upande
wa Mashariki hadi wa Magharibi. Kama Green
Crescent, sisi ndio wasidizi wakubwa zaidi wa vijana
wetu na familia zao, tukishiriki katika kuzuia uraibu
wamadawa ya kulevya na ukarabati wa waraibu, na
kutoa msaada kuwafanya warudi na waanze kuishi
na bidamu wengine au kujumuishwa tena kwenye
jamii. “
MKAKATI WA ISTANBUL
Mkutano wa kwanza, Istanbul, Tarehe 12-13 JunI 2019
TAMKO
1. Idadi kubwa zaidi ya watu duniani hawatumii
madawa ya kulevya na wanataka kuishi kwenye
mazingira yasiyo na hatari zinazotokana na
kulewamadawa. Kundi hili ambalo ndilo kubwa
zaidi duniani linaunga mkono shughuli za
kuzuia ulevi wa madawa pamoja na kuwezesha
vijana na watu wengine walio hatarini kukuza
mikondo ya maisha, desturi na mazingira yenye
afya ili kuhakikisha upatikanaji wa afya bora na
maendeleo kwa wote.
2. Sisi, ambao ni wawakilishi wa mashirikia
yasiyo ya kiserikali ya kimataifa na ya kieneo
tuliotia saini hapo chini,
3. Tunatambua kwamba utumiaji pombe,
sigara, madawa ya kulevya na vifaa vinginevyo
vinavyochanganya akili husababisha madhara
ya kiafya, kijamii na kiuchumi kwa watu binafsi,
familia zao, jumuiya zao na jamii zao kwa jumla
na hatimaye kuhatarisha maendeleo endelevu.
4. Tunatanguliza afya na maslahi ya binadamu
wote, na kwa hiyo, tumesanyika kwenye
mkutano wa kwanza wa Mkaatati wa Istanbul
kutoa uamuzi kuhusu mahitaji ya vitendo vya
dharura vya kusuluhisha tatizo la madawa ya
kulevya duniani, mkiwemo ulevi wa vifaa na
tabia zinazochanganya akili;
5. Tunasisitiza kwamba kupunguza kiwango
cha upatikanaji wa madawa ya kulevya na
kuhakikisha kiasi chake kinakuwa chini sana
ndiyo njia bora zaidi ya kutoa kinga. Kutoa
kinga dhidi ya madhara ndiyo njia iliyo nafuu
zaidi inayozingatia utu na iliyo endelevu katika
kupunguza madhara yatokanayo na utumiaji
wa madawa ya kulevya, kuokoa masiha,
kuimarisha jumuiya mbalimbali, kukuza afya
ya jamii, maendeleo endelevu ya binadamu na
kupunguza matatizo yanayohusiana na ulevi.
6. Tunatambua kwamba sera za kukumbana
na madawa ya kulevya lazima zitungwe kwa
kuzingatia haki za kibinadamu, jinsia na umri;
7. Tunasisitiza umuhimu wa kuweka mifumo
ya kimatibabu inayolenga kuinua afya ya
wagonjwa wa ulevi, masuluhisho yanayojali
kila hali ya mgonjwa, kuanzia masuluhisho ya
awali hadi kupunguza madhara, kukarabati na
kumwezesha mgonjwa kukubaliwa tena katika
jumuiya yake, kwa lengo la kuwasaidia watu
walioathiriwa vibaya na utumiaji madawa ya
kulevya ili waweze kuishi maisha yenye fanaka.
8. Tunatambua
kwamba
madhara
yatokanayona na utumiaji madawa ya kulevya
hayaathiri tu mtu binafsi lakini pia yanaathiri
vibaya wachumba wao, wazazi wao, ndugu zao
na watoto wao; na kwa hiyo huduma thabiti za
usaidizi kwa familia na kwa watu wa uhusuano
wa karibu na mlevi wa madawa ni wa muhimu
sana katika kuzuia madhara na kujenga
misingi imara ya familia zenye stahamala;
9. Tunasisitiza umuhimu wa ushirika wa
wanajamii wote katika kukabili matatizo ya
utumiaji madawa ya kulevya kama jukumu la
kila mtu linalohitaji kukabiliwa kwa pamoja
kwa kuegemea ushahidi wa utafifi ili kubadili
sera, itikadi na mifumo katika viwango vyote
kupitia ushirikishaji wanajamii;
10.Kwa sikitiko kubwa tunafahamu hatari
za biashara za pombe na sigara, na sasa
tunasikitika zaidi kuona uibukaji wa biashara
mpya inayokuza utumiaji madawa ya kulevya
kwa faida ya watu binafsi, na kusababisha
madhara ya ajabu hasa kwa makundi ya watu
dhaifu na jamii kwa jumla.
11. Tunasikitika sana kuona biashara hii mpya
imeweza kupotosha ukweli na kuelekeza sera
za umma na kushawishi serikali, mashirika
ya kimataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali
mbalimbali kwa ajili ya kufaidika kiuchumi,
kinyume na maslahi ya wanajamii;
12.Tunapigia mbiu watu wote, hasa viongozi
wa familia, kisiasa, kitamaduni, kidini, kiraia,
kiafya, kielimu, vijana, michezo, na biashara, na
vyombo vya habari kushiriki kwenye harakati
za kugeuza itikadi za kijamii, kupunguza
upatikanaji wa madawa ya kulevya, na kujenga
jamii zenye afya bora;
13. Tunapigia mbiu serikali zote na jumuiya ya
kimataifa kushikilia mkabala unaosawazisha
pembe zote za kupunguza kiasi na idadi ya
watumiaji madawa, kupunguza kiwango cha
uingizaji madawa na mamlaka za kuhakikisha
utendekaji wa sheria, na kuwekeza kwenye
harakati za kuzuia, kutibu na huduma za afya,
ili kufaulu katika kupata utulivu na ulinzi wa
kimataifa, na afya njema kwa mataifa;
14. Tunapigia mbiu serikali zote kuwekeza
kwenye mazingira yanayokuza afya bora ili
kufaulu katika kupata afya inayotamanisha,
neemai na maendeleo kwa watu wote;
15.Tunatamka nia yetu ya kuzidi kushirikiana
duniani kote kuunga mkono mipango
inayoshirikisha wanajamii wenyewe kwenye
mchakato wa utungaji sera wa kimataifa na
kupaaza sauti za kundi lililo kubwa zaidi la
wanajamiii wasiotumia madawa duniani kote.
43