

wanaowazunguka katika mapambano
dhidi uraibu wa madawa ya kulevya. Kila
kazi inayowasilishwa kwa mashindano
haya ni muhimu sana kwetu, kwani ni
ya thamani sana kwetu kwamba wana
uwezo wa kuunda kazi inayoonyesha
mapambano dhidi ya uraibu wa madawa
ya kulevya na kuweza kushindana katika
umri huo mdogo. Tena, ningependa
kumshukuru kila mtu ambaye alishiriki.
Ikiwa hatutaki watoto wetu wakue na
kuwa watu wazima wachukivu, lazima
tuanze mapambano mapema wangali
bado umri mdogo na kuwakuza wakiwa
watu wenye furaha na wenye afya njema.
Sisi kama Green Crescent, tunaendelea
kufanya kazi hadi mwisho na tunatarajia
msaada wako. “
“Utakuwa na mahali katika paa la
Green Crescent Daima”
Mwanachama wa Bodi ya Green Crescent
Dkt. Esra Albayrak alitumia fursa katika
hafla ya kutunukia washindi tuzo
kusisitiza mahitaji ya kutekeleza shughuli
kama hizo: “Shughuli kama hizo ni jukumu
kwetu. Ushiriki wa vijana wetu unahitaji
mapenzi makubwa. Tunamshukuru kila
mtu. Tunapenda kuwashukuru watoto
wetu wapendwa na vijana, na pia walimu
wanaowaunga mkono na kila mtu
anayewasaidia vijana. Nikupongezeni,
na
kukutakia
fanaka.
Ningependa
kukukumbusheni kuwa daima utakuwa
na mahali chini ya paa la Green Crescent.
Siku zote tuko hapa, kama kaka na dada
zako. “
Mashindano yameenea kote nchini
kwa miaka 3 iliyopita
Prof Ahmet Emre Bilgili, Mkurugenzi
Mkuu wa Elimu Maalum ya Huduma za
Ushauri Nasaha katika Wizara ya Elimu ya
Kitaifa (MONE), alisema kwamba uraibu
wa madawa ya kulevya ulikuwa ni moja
wapo ya changamoto kubwa ulimwenguni
leo, ukiwatisha watu na jamii.
Alibaini kuwa mashindano ambayo
yamekuwa
yakifanywa
juhudi
za
ushirikianowaWizara ya Elimu ya Taifa na
Green Crescent kwa miaka tisa yamefikia
hatua muhimu sana, yakiwa yameenea
kote nchini katika miaka mitatu iliyopita
baada ya kufanyika tu Istanbul kwa miaka
sita.
Zaidi ya kazi 185,000 ziliwasilishwa
Washindi wa kimkoa wa mashindano
ya vipaji ya”Kazazi chenye Afya njema,
Afya ya bora ya Baadaye”” walipewa tuzo
ya kifedha ya lira 500 kwenye sherehe
zilizofanyika katika majimbo yao. Katika
fainali, washindi walipewa Lira 5,000,
wakati wale waliochukua nafasi ya pili
walipokea lira 3,000 na wale waliochukua
nafasi ya tatu walipokea lira 1,500 za
Uturuki.
İdil Dilara Kahramano lu
Mshindi wa shindano la Sanaa ya uoni la Shule za Sekondari ya juu
Asya Makbule Kılıç
Mshindi wa shindano la Sanaa ya uoni la Shule za Msingi
Ya mur Albayrak
Mshindi wa shindano la Sanaa ya uoni la Shule za
Sekondari ya chini
49