

Lebanon Green Crescent – Shirika
la Stardom
• Shina la Green Crescent nchini
Lebanon lilianzishwa mwaka 2016.
• Uvutaji sigara na madawa ya
kulevya ndizo aina za ulevi za hatari
zaidi nchini Lebanon.
· Shughuli za Shina la Green Crescent
nchini Lebanon ni pamoja na:
- Maandalizi ya “Kongamano la
Matumizi ya Intaneti kwa mtazamo
wa Kulewa” kwa ushirikiano na
Wizara ya Mambo ya Kijamii ya
Lebanon.
- Mikutano ya kutoa mafunzo kuhusu
kulewa inayohisisha wanafunzi
700,000 kutoka shule 25.
- Maandalizi ya kampeni ya
uhamasishaji yenye kichwa “Tarehe
31 Mei Siku ya Kutovuta Sigara” kwa
ushirikiano na Munisipali ya Tripoli.
- Kulianzishwa mradi wa “Basi la
Uhamasishaji” ili kuhamasisha
jamii juu ya kulewa na kuhakikisha
matibabu ya haraka sana.
Montenegro Green Crescent -
Zeleni Polumjesec
• Shina la Montenegro Green Crescent
lilianzishwa mwaka 2014.
• Uvutaji sigara na utumiaji pombe
ndivyo vilevyo vya hatari zaidi
nchini Montenegro.
· Shughulinza Montenego Green
Crescent ni pamoja na:
- Chini ya mradi “Kuzuia Uvutaji
sigara katika shule za Sekondari”,
shina lilifanya uchunguzi katika
shule nne katika eneo la Popdorica
na kuwasilisha matokeo yake
kwa wanafunzi hao kupitia
makongamano.
- Kuliandaliwa kongamano kuhusu
kulewa katika Chuo Kikuu cha
kiserikali cha Montenegro, Ndaki ya
Sheria.
- Rais wa Montenegro Green Crescent
Amer Halilovic alifanya ziara
kwa Ofisi kuu za Shirika la Green
Crescent nchini Uturuki.
Green Crescent nchini Bosnia and
Herzegovina
• Green Crescent nchini Bosnia &
Herzegovina lilianzishwa mwaka wa
2014.
• Unywaji pombe ndio ulevi wa hatari
zaidi nchini Bosnia & Herzegovina.
· Shughuli za Bosnia & Herzegovina
Green Crescent ni pamoja na:
- Warsha juu ya madhara ya utumiaji
madawa, pombe na sigara katika
shule za sekondari ya chini nay a juu.
- Warsha juu ya madhara yanayoletwa
na utumiaji madawa ya kulevya,
pombe na kuvuta sigara katika shule
za kidini.
Georgia Green Crescent -
Gürcistan Yeşilay Cemiyeti
• Chama cha Green Crescent nchini
Gerogia kilianzishwa mwaka wa 2015.
• Alcohol is one of the leading
addictions in Georgia. Ulevi wa
pombe ndio ulevi wa hatari zaidi
nchini Georgia.
· Shughuli za shina la Georgia Green
Crescent ni pamoja na:
- Chini ya “Mpango wa Kubadilishana
Tajriba” wa Awamu ya Uturuki
ya Ushirikiano na Uratibu (TIKA),
mkutano wa uhamasishaji ulifanywa
kwa watumishi wa kujitolea
waliokuja nchini Georgia kwa ajili ya
mpango huu.
- Kulifanyika onyesho kwenye ukumbi
wa maonyesho wa Marneuli nchini
Georgia kuhamasisha watu juu ya
ulevi. Onyesho hili lilivuta watu 270,
mkiwemo mawakala kutoka Ubalozi
wa Uturuki nchini Georgia, Tbilisi
TIKA, Chuo cha Yunus Emre na
MUSIAD.
- Mijadala kati ya shina na Shirika la
Ujdhibiti wa Sigara la Georgia, na
kupata ushauri kuhusu utekelezaji
wa miradi iliyopangwa.
- Kuandaliwa kwa mkutano wa
uhamasishaji wenye mada “Mbinu za
Kukabili Ulevi”.
- Kufanya ziara kwa shule za awali
kukuza mienendo ya kiafya katika
Siku ya Watoto ya Dunia.
Bulgaria Green Crescent - Yeşilay
Bulgaria
• Shina la Bulgarian Green Crescent
lilianzishwa mwaka wa 2015.
• Ulevi wa pombe ndio ulevi wa
hatari zaidi nchini Bulgaria.
· Shughuli za shina la Bulgarian
Green Crescent ni pamoja na:
- Warsha kadhaa kuhusu ulevi wa
teknolojia na madhara yake wakati
wa Wiki ya Green Crescent.
- Kongamano kuhusu kulewa
teknolojia.
- Sherehe ya iftar iliyohudhuriwa
na Balozi wa Jamhuri ya Uturuki
nchini Bulgaria na Mufti Mkuu wa
Jamhuri ya Bulgaria.
Green Crescent Indonesia
• Shina la Green Crescent Indonesia
lilianzishwa mwaka wa 2016.
• Uvutaji sigara ni mojawapo ya
hatari kubwa za ulevi nchini
Indonesia.
· Shughuli za Green Crescent
Indonesia ni pamoja na:
- Mikutano ya uhamasishaji juu ya
mada “Kuacha Sigara” katika shule
22.
- Kuliandaliwa kongamano la “Dunia
ya Ulevi 2018”
- Uanzishaji wa Jarida la Vizazi
(Generation Magazine) lenye lengo
la kuwasaida vijana kujitenga na
aina zote za ulevi.
- Wasilisho kwenye Rediyo ya
Kiislamu ya Suara juu ya shina la
Green crescent la Indonesia.
- Maandalizi ya warsha kuhusu
uvutaji sigara katika Chuo Kikuu
cha Surabaya, ndaki ya elimu-Tiba,
Idara ya matibabu ya kiakili.
53