

Shina la Green Crescent la Moroko
جمعية الهلال الأخضر المغربي
• Shina la Green Crescent nchini
Moroko lilianzishwa mwaka wa
2018.
• Uvutaji wa sigara na bangi ndio
ulevi wa hatari zaidi nchini
Morocco.
· Shughuli za shina la Green
Crescent la Moroko ni pamoja na:
- Kushiriki kwenye kongamano
juu ya mada “mdahalo wa Kitaifa
kuhusu Sera za madawa ya kulevya
na Mashirika yasiyo ya kiserikali”
lililoandaliwa na Wizara ya
Mashirika ya Kibinafsi.
- Mkutano wa kimawasiliano
uliokuwa kati ya shina na
mashirika mbalimbali kwenye
Kituo cha Vijana cha Munisipali ya
Bouskoura.
- Maandalizi ya Kongamano la
Kimataifa la Ulevi.
Chama cha Green Crescent nchini
Somalia - Bisha Cagaaran ee
Soomaaliaya
• Shina la Green Crescent nchini
Somalia lilianzishwa mwaka wa
2015.
• Utumiaji madawa ya kulevya
ndiyo hatari kubwa ya ulevi katika
jamiiya kiSomali.
· Shughuli za shina la Green
Crescent la Somalia ni pamoja na:
- Mikutano ya mafunzo ya
uhamasishaji juu ya ulevi.
- Mikutano iliyotendeka na wadau
kama Ubalozi wa Somalia nchini
Uturuki, TIKA, Wizara mbalimbali,
asasi za kidini na vyama vya
wanafunzi.
- Vitendo vya kuhamasisha jamii
kuhusu kulewa.
- Maandalizi ya mpango kwenye
rediyo wa uhamasishaji juu ya
ulevi.
Shina la Green Crescent la
Malaysia - Pertubuhan Bulan Sabit
Hijau Malaysia
• Shina la Green Crescent la Malaysia
lilianzishwa mwaka wa 2016
• Uvutaji sigara ni mojawapo ya ulevi
hatari zaidi nchini Malaysia.
· Shughuli za shina la Green
Crescent la Malaysia ni pamoja na:
- Kozi na mafunzo yaliyotolewa kwa
watumishi wa kujitolea chini ya
mpango wa “green Crescent kwa
Vijana”
- Kwenye tamasha la michezo ya
mtandaoni, shina lilianzisha
jukwaa la kuwaonya vijana hatari
za ulevi wa intaneti.
- Maandalizi ya Kongamano la Afya
la Kimataifa
- Kwenye Siku ya Dunia ya Ugonjwa
wa Kifikira, jukwaa lilianzishwa
kuhamasisha vijana kuhusu tabia
za ulevi.
Shina la Green Crescent la Serbia -
Zeleni krst -Zeleni polumsejec
• Shina la Green Crescent nchini
Serbia lilianzishwa mwaka wa 2016.
• Pombe ndio ulevi wa hatari zaidi
nchini Serbia.
· Shina la Green Crescent la Serbia
lina shughuli zifuatazo:
- Kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa
shule za msingi kuhusu ulevi na
hatari zake.
- Warsha zinazofanyika shuleni
kuhusu “Athari za Utumiaji sana
simu na kutazama skrini”
- - Warsha ziliandaliwa chini ya
mradi wa “Elimu ndiyo Kinga
Bora zaidi”, juu ya hatari za sigara,
pombe na utumiaji madawa ya
kulevya.
Shina la Green Crescent la Sudani
جمعية الهلال الأخضر السوداني
• Shinala Green Crescent la Sudani
lilianzishwa mwaka wa 2014.
• Utumiaji madawa ya kulevya ndio
ulevi wa hatari Zaidi cnhini Sudani.
· Kazi za shina la Green Crescent la
Sudani ni pamoja na:
- Kampeni za uhamasishaji
zilizoanzishwa katika shule sita
kwa kushirikiana na idara za Elim
- Mijadala ya pamoja iliyofanyika
na Bunge ya Sudani, Awamu
mbalimbali za Kiserikali na
mashirika yasiyo ya kiserikali.
Shina la Green Crescent la
Zimbabwe
• Shina la Green Crescent nchini
Zimbabwe lilianzishwa mwaka wa
2015.
• Sigara, pombe na madawa ya
kulevya ni miongoni mwa ulevi wa
hatari zaidi nchini Zimbabwe.
· Shina la Green Crescent la
Zimbabwe linatekeleza shughuli
zifuatazo:
- Sherehe ya Wiki ya Green Crescent
pamoja na Shirika la Madaktari la
Zimbabwe.
- Kushiriki kongamano lililoandaliwa
kwenye Chuo Kikuu cha Kiserikali
cha midlands.
- Maandalizi ya paneli ya kujadili
tabia za ulevi iliyohudhuriwa na
wataalam wa ugonjwa wa akili.
- Kushiriki kwenye warsha juu ya
ulevi iliyoandaliwa na Kanisa
la Zenzega, ambapo jukwaa
lauhamasishaji lilifunguliwa na
watu kuhutubiwa.
55