

“Kila mtu ana sababu ya kuwa na
Afya bora”
Shirika la Green Crescent ni mfano
wa kuigwa duniani kwa sababu ya
kazi zake. Shirika hili linajiandaa
kusherehekea
kumbukumbu
ya
miaka 100. Rais Prof. Mücahit Öztürk
katika hotuba yake kabla ya ziara
hiyo alisisitiza ya kwamba kuishi
maisha bora kiafya inawezekana kwa
kuepukana na dawa za kulevya. Prof.
Mücahit Öztürk alisema, “Uwanja wa
kupambana dhidi ya dawa za kulevya
umepanua. Athari za uhamasishaji
wetu zinashika moto kila kukicha.
Kwa niaba ya Green Crescent,
ningependa kushukuru kila mtu
ambaye ameshiriki katika ziara ya
uendeshaji baiskeri ya mila yetu ya
Green Crescent, na nyote mliotusaidia
katika mapambano haya. Kwa mara
ya 10 ya uendeshaji baiskeli,ya mwaka
2020, tutaendelea kuendesha baiskeli
kwa shauku nyingi.” Akisema kwamba
kila mtu anayejiunga na ziara za
kuendesha baiskeli ana kila sababu
ya kuishi vizuri, Prof.Mücahit Öztürk
alishukuru washiriki wote kwa muda
wao.
Maelfu Wahudhuria
Murat Suyabatmaz, Rais wa Chama cha
Wapanda baiskeli, alisema kwamba
ushiriki katika ziara ya kupanda
baiskeli ya Green Crescent imekuwa
ukiongezeka kwa kasi. : “Tumeungana
hapa katika Kioski ya Basketmakers’
siku hii ya Jumapili kwa mara ya tisa
ili kukuza mtindo wa maisha ya kiafya
ya Green Crescent. Mwaka huu pia,
tunapanda baiskeli mara nyingine
kupiga vita dhidi ya utumiaji wa dawa
za kulevya kama tufanyavyo kila
mwaka”
Washiriki wazawadiwa na baiskeli
Burak Arslan, ambaye ni mwenyeji
wa tukio aliwakumbusha washiriki
kwamba Green Crescent ni shirika
lisilo la Kiserikali na kubwa nchini
linalojishughulisha
sana
na
mapambano dhidi ya dawa za kulevya
ambalo ni mojawapo ya tatizo kubwa
nchini Uturuki. Wakati wa ziara
ya kuendesha/ kupanda baiskeli,
washiriki kumi walizawadiwa na
baiskeli baada ya kushinda bahati
nasibu.
59