

“Green Crescent ni kituo cha
suluhisho na matibabu katika
mapambano dhidi ya Uraibu
wa madawa ya kulevya.
Rais wa Green Crescent Prof.
Mücahit Öztürk alimshukuru
Rais Recep Tayyip Erdoğan kwa
usaidizi wake na kuwapongeza
watu
na
mashirika
waliozawadiwa kama “Wasaidizi
wazuri
zaidi
wa
Crescent
yaani “Best Green Crescent
Supporters”.
Akiendelea
na
houba yake katika sherehe, Prof.
Öztürk alisema, “Tunatekeleza
jukumu la kukinga, kulinda na
kukarabati shughuli za afya ya
jamii ili kuhamasisha kuhusu
uraibu wa madawa ya kulevya.
Leo Green Crescent inaaminiwa
sio tu nchini Uturuki bali
duniani kote. Kwa kuongezea,
ni kuchukua hatua muhimu
kuwa kituo cha suluhuhisho na
matibabu kwa kuwa na shughuli
anuwai zinazohusiana na afya ya
jamii. Kufikia sasa, tunapanua
eneo na kazi za Kituo cha
Mafunzo na Ushauri cha Green
Crescent yaani; Green Crescent
Training
and
Counseling
Center (YEDAM) kutoa huduma
za kiakili naukarabati kwa
watawaliwa/waraibu wa pombe
na madawa ya kulevya pamoja
na familia zao. Zaidi ya hayo,
kama Mfano wa Ukarabati wa
kitaifa, tunaanzisha Kituo cha
Ukarabati cha Green Crescent
baada ya kutathmini vituo hivyo
katika nchi 20 kama vituo vya
pamoja vya kutibu na kuponea
kwa watawaliwa/waraibu wa
madawa ya kulevya.
“Wasaidizi Bora zaidi wa
Green Crescent” wapewa tuzo
Katika sherehe ya kutoa zawadi/
tuzo ya 5 ya kifahari ya Phoenix
mwaka huu, tuzo ilipewa kwa
Mevlüt Uysal, meya wa Manispaa
ya Istanbul katika kategoria ya
siasa, kwa Ceza katika Sanaa,
Kwa Bobby Dixon Ali Mohammed
katika michezo, kwa to Prof.
Marc Potenza katika taluuma,
NTV katika kategoria ya vyombo
vya habari na kwa Turkcell kwa
wajibu wa Umma.
Maonyesho ya Mpiga Picha Mashuhuri
Bispuri ya “Hadithi Fiche”
Mwishoni mwa Kongamano la kimataifa la
2 la Sera ya Madawa ya Kulevya na Afya ya
Umma lililofanywa na Green Crescent, tarehe
26-28 mwaka wa 2018, hatari za utumiaji wa
madawa ya kulevya zilionyeshwa kupitia
picha za mpiga picha maarufu kutoka Italia,
Valerio Bispuri. Maonyesho ya Bispuri ya
“Hadithi Fiche” yaliegemezwa kwenye dhana;
“Kwa ajili ya Ubinadamu” na kuonyesha
madawa ya kulevya na hatari zake kwa
msimamo wa ‘msanii’. Katika maonyesho,
Bispuri alielezea uharibifu unaofanywa na
madawa ya kulevya kwa jamii na watu binafsi
akitumia moto unaoungua na kuonyesha
jinsi hasara inayosababishwa na madawa
ya kulevya haibagui taifa au rangi, haswa
kupitia picha zake za kushangaza za watu
wanaoishi katika vitongoji vya Marekani
Kusini.
Bispuri alisema kuwa alifurahi sana kupata
fursa ya kuonyesha picha zake katika
muktadha muhimu katika Kongamano la
Kimataifa la 2 la Sera ya Madawa ya Kulevya
na Afya ya Umma: “Wakati nilipopiga picha
hizo, niliona athari kubwa ya uraibu wa
madawa ya kulevya, watu walioteseka.
Nilishuhudia kwamba ubaya unaofanywa na
uraibuwamadawa ya kulevya haujui mipaka,
rangi au mataifa, “alisema Bispuri. Valerio
Bispuri ameshinda tuzo nyingi, pamoja na
Siku ya 9 ya Japani mnamo 2013, Tuzo ya
Uandishi wa Habari wa Kimataifa na Tuzo ya
Dunia ya Upigaji picha ya Sony mwaka 2013
katika kategoria ya “Maswala ya Kawaida”.
Maonyesho ya “Chini ya chupa” na Green
Crescent
GreenCrescent,katikaWikiyaUhamasishajiwa
Pombe, walishiriki maonyesho ya kushangaza
na kuonyesha uharibifu uliosababishwa na
pombe, kwa mtu binafsi na kwa jamii, yenye
jina la “Chini ya chupa”. Maonyesho hayo,
ambayo yalifanyika katika sehemu nyingi za
katikati mwa Istanbul, mmoja wapo ya miji
mikubwa duniani, hufanya kazi muhimu
katika kuonyesha athari za unywaji wa pombe,
kusababisha dhuluma katika jamii. Maonyesho
hayo yalitolewa kwa umma huko Karaköy Pier
na msaada wa City Lines mnamo Novemba
21-25, 2018, kwenye maktaba ya Beyazıt State
tarehe 15 Machi 2019 na katika Maktaba ya
Umma ya Wilaya ya Gaziosmanpaşa tarehe 3
Juni, 2019
Uraibu wa madawa ya kulevya kama
ulivyochorwa na wachoraji katuni wa
Kimataifa
Green Crescent iliwasilisha kazi bora kwa
wakaazi wa Istanbul katika Mashindano ya
Katuni ya Green Crescent, ambayo yaliandaliwa
ili kuongeza uhamasishaji wa uraibu wa
madawa ya kulevya kwa umma. Kazi bora
kabisa zilizoingia katika Mashindano ya tatu ya
Katuni ya Green Crescent , ambapo washiriki
414 kutoka nchi 51 waliwasilisha jumla ya kazi
787, zilizoonyeshwa katika vituo vya kuvutia
vya Istanbul. Maonyesho hayo yaliwatia sana
watu huko Kadıköy Square mnamo Machi 1-7,
2019; kwenye vivuko vya Mji wa Istanbul tarehe
9 Februari 2019; katika Kituo cha Utamaduni
cha Istanbul Caddebostan tarehe 16-19 Julai,
2019; katika Kituo cha Ununuzi cha Istanbul
Tepe Natuilus tarehe 20-27 Julai, 2019; katika
barabara ndogo ya Istanbul Kadıköy kati ya Mei
29-Juni 5, 2018; katika Ukumbi wa Tamasha wa
Cemal Reşit Rey mnamo Aprili 20, 2018, nk.
GREEN CRESCENT HUKUZA
UHAMASISHAJI KUPITIA
SANAA YA UCHORAJI
Green Crescent hupitia kwenye uwezo wa jamii wa Sanaa
ya uchoraji kufichua maadhara ya uraibu wa madawa ya
kulevya ya kushtua. Kusudi lake ni kukuza uhamasishaji
wa uraibu wa madawa ya kulevya katika jamii kupitia
maonyesho yanayofanywa kitaifa na kimataifa.
63