Background Image
Previous Page  66 / 68 Next Page
Information
Show Menu
Previous Page 66 / 68 Next Page
Page Background

Michezo ya mtandaoni duniani na kamari ya mtandaoni, uraibu wa

kamari hutishia sana vijana na watoto mahusisi. Tulizungumza na

Dkt. Marc Potanza kutoka Idara ya Magonjwa ya Akili wa Chuo

Kikuu cha Yale Shule ya Dawa kuhusu mabadiliko yanayoonekana

katika uraibu wa uchezaji Kamari na hatua zinazohitaji

kuchukuliwa.

Je! Ungetathmini vipi hali ya sasa ya

dunia kuhusu uraibu wa kamari?

Uraibu wa kamari, kama istilahi rasmi

ya uraibu wa kamari, umeainishwa

hivi karibuni katika Utambuzi na

Mwongozo wa Takwimu ya magonjwa

yaakili DSM-5na ICD- 11 yaani Uanishaji

wa Kimataifa wa magonjwa kama

uraibu wa kitabia. Ingawa uchezaji

wa kamari umekuwa mojawapo wa

tamaduni nyingi duniani kwa miaka

mingi,

kuna

mabadiliko

mengi

ambayo yametokea na kubadilisha

tabia za uchezaji kamari. Kwa mfano,

kamari za mtandaoni zimeongezeka

sana katika muongo mmoja uliopita,

na mbinu ambazo watu hucheza

kamari ya mtandaoni hutofautiana

na njia wanazocheza wasipokuwa

mtandaoni, kwa sababu ya sehemu

ya utaftaji na upatikanaji. Aidha,

uchezaji wa kamari na kamari ya video

vinakaribiana kisifa, kuwalinda vijana

kutokana na mabadiliko kutoka kwa

michezo ya kubahatisha na kuanza

kucheza kamari, na kisha kwa uraibu

wa kamari, ni janbo muhimu sana.

Je, nini kinafanywa kulinda afya

ya jamii. Je, kuna mpango gani kwa

maisha ya badaye?

Mamlaka

tofauti

ya

kisheria

yamechukua mikakati tofauti kulinda

afya ya jamii. Baadhi ya nchi zimepiga

marufuku michezo ya kubahatisha

na kamari kwa ujumla, nchi nyingine

zinajitahidi kuongeza kodi ya kamari

na kuiwekea viziwizi kadhaa; na katika

nchi nyingine kamari haikudhibitiwa

hata kidogo. Shirika la Afya Duniani

lilitoa fasili ya kamari iliyokithiri

katika ICD-11, likilenga kushughulikia

tabia hatari za kamari ambazo

hazijakuwa kufika katika kiwango

cha uraibu wa kamari. Kwa miaka

mitano iliyopita, shirika la Afya

Duniani limekuwa likikutana kujadili

maendeleo ya vyombo ya kutathmini

vya michezo inayojihusisha na Kamari

ambavyo vinaweza kutumiwa katika

mamlaha tofauti ya kisheria.

Mashirika ya kijamii hufanya

majukumu gani katika uwanja huu?

Wadau wengi wapo; na lazima

washiriki katika uthibiti wa uraibu

wa kamari na katika kuwasiadia watu

walio na hali hiyo. Ni lazima makundi

yanayojihusisha katika utoaji wa

huduma za kamari (yale ya serikali na

yasio ya serikali) yalenge kulinda afya

ya jamii. Kuelewa uwezo wa athari za

kamari haswamiongoni mwamakundi

yanayoweza kuathiriwa na Kamari ni

muhimu sana katika mchakato huu.

Watunga sera wanapaswa kutunga na

kutekeleza sheria zinazolinda watu

kupata shida zinazohusiana na Kamari

na kusaidia shughuli zinazosaidia

watu ambao wamepata shida kama

hizo.

Mashirika

yanayodhamini

utafiti katika kinga, kutibu na afya

ya jamii yatoe msaada wa kutosha

kwa utafiti unaohusiana na kamari.

Ni lazima Maofisa wa Afya ya Jamii na

wotoa huduma ya Afya, wafundishwe

kuhusu uraibu wa kamari na njia bora

ya kuuzuia na kuutibu.

Una maoni gani kuhusu shirika

la Green Crescent na juhudi zake

katika eneo hili?

Green Crescent limekuwa shirika

tendaji katika kushughulikia uraibu

wa kamari katika pande nyingi. Jamii

ya Green Crescent imedhamini na

kujihusisha na majaribio ya shirika

la Afya Duniani zinazolenga to

kushughulikia tishio la Kamari. Shirika

la Shirika la Green Crescent limekuwa

likifanya kazi ikiwa na kushughulikia

shida za kamari kwenye pande nyingi.

Jumuiya ya Green Crescent imeunga

mkono na imekuwa ikihusika na

Shirika la Afya Duniani ikilenga

kuthibiti kushughulikia kimari

hatari sana. Shirika la Green Crescent

limetoa mafunzo katika uzuiaji na

matibabu ya shida za kamari nchini

Uturuki. Kupitia juhudi kama hizo,

afya ya jamii nchini Uturuki na kote

duniani itaboreshwa.

Mahojiano na: Kemal Altın

DKT. MARC POTANZA;

“UCHEZAJI KAMARI

MTANDAONI HUCHOKO

A URAIBU”

Dkt. Potanza ni mhadhiri katika

Idara ya Magonjwa ya Akili ya Chuo

Kikuu cha Yale Shule ya Dawa. Yeye

ni Mkurugenzi wa Idara ya Nyurolojia

Kituo cha elimu ya watoto, kituo

cha Utafiti kuhusu Kamari, mpango

wa uchunguzi kuhusu udhibiti wa

ugonjwa unaosabisha mhemko wa

ghafla pamoja na kufanya utafiti wa

wanawake na Uraibu na kiini cha Afya

ya Wanawake katika Chuo kile kile.

JE, DKT. MARC POTANZA NI NANI?

64