

Kupitia Mpango wa Kimataifa wa Ukufunzi, Green Crescent inawapa
wanafunzi kutoka nchi mbalimbali fursa ya kujiunga na ukufunzi ili
wapate uzoefu wa kufanya kazi wakiwa pamoja na wale wanaohusika
katika mapambano dhidi ya ulevi wa madawa. Wakati ikiwapa
wanafunzi ujuzi kuhusu jitihada za kupambana na ulevi wa madawa,
Mpango huo pia utachangia ukuaji wao wa kibinafsi na wa kitaaluma.
MPANGO WA KIMATAIFA
WA UKUFUNZI WA
GREEN CRESCENT
G
reen Crescent imezindua Mpango
wa Kimataifa wa Ukufunzi ili
kusaidia wanafunzi kupata uzoefu
wa kufanya kazi pamoja na wale
wanaohusika
katika
mapambano
dhidi ya ulevi wa madawa. Mpango
wa Kimataifa wa Ukufunzi unawapa
wanafunzi kutoka nchi mbalimbali
ulimwenguni fursa ya kuelewa na
kuchangia shughuli za Green Crescent,
ikiwapatia pia uzoefu katika shughuli
za kinga, afya ya umma na utetezi
za kinga na urekebishaji. Wanafunzi
wa saikolojia, afya ya umma au
mawasiliano au wahitimu wapya
wanapata ufahamu katika uwanja
wa kupindana na ulezi, na hivyo
kuchangia maendeleo yao ya kibinafsi
na ya kitaaluma.
Fursa ya kupata uzoefu katika
urekebishaji
Wanafunzi
watapewa
majukumu
mbalimbali, kulingana na usuli wao
wa elimu, uzoefu wao wa zamani na
upendeleo wao, na watapata fursa ya
kupata uzoefu, hasa katika uwanja
wa urekebishaji. Waombaji waliofaulu
watahudhuria mipango ya mafunzo
pamoja na mahojiano yanayohusisha
walevi wa madawa katika Kituo cha
Green Crescent cha Mafunzo na
Ushauri, ambapo shirika hili linatoa
huduma za bure za kisaikolojia na
kijamii za bure kwa walevi wa madawa
na jamaa zao. Wakufunzi pia watapata
nafasi ya kushiriki katika miradi
mbalimbali. Zaidi ya hayo, mpango huo
unawapa wanafunzi fursa ya kipekee
ya kukuza uwezo katika uwanja wa
matibabu ya ulevi wa madawa, kupata
ujuzi wa masuala husika ya kijamii, na
kugundua tamaduni mpya na mitindo
ya maisha kupitia ujifunzaji na watu
wa rika lao.
50