

Prof. Mshiriki, Dakt. Perihan Torun ambaye ni kiongozi wa utafiti wa
sera za Uturuki kuhusu Udhibiti wa Pombe wa Kimataifa, alisema:
“Madai kwamba kuna manufaa yanayotokana na kutumia kiasi fulani
cha pombe hayana mashiko, kwani uchunguzi uliofanyika hivi juzi
umekadiria kwamba mzigo wa dunia wa maradhi yanayotokana na
utumiaji pombe yanaongezeka sambamba na ongezeko la kiasi cha
pombe kinachotumika.”
Ungefafanuaje kiasi cha pombe
kinachotumika duniani hivi sasa?
Shirika la afya la Dunia (WHO)
limeripoti kwamba takribani nusu ya
watu duniani wenye umri wa miaka
15 na zaidi hawajawahi kuonja pombe.
Pombe inatumiwa na zaidi na nusu ya
watu katika maeneo ya WHO matatu
kati ya sita, yaani maeneo ya Bara
ya Amerika, Ulaya na Mashariki ya
bara ya Pasifiki ambako utumiaji
pombe huanza kabla ya mtu kutimia
umri wa miaka 15. Katika miaka
michache iliyopita, kiasi cha pombe
kinachotumiwa kinasemekana kuwa
kinaongezeka katika maeneo ya WHO
ya kusini-magharibi ya Pasifiki na
Kusini ya Asia, na kupunguka katika
eneo la Ulaya.
Nchi zenye idadi ya chini ya
watumiaji pombe, zile zisizo na
sera kali za kudhibiti pombe na/
au zisizotekeleza sera za kudhibiti
pombe zina nafasi kubwa ya kuvuta
kampuni zinazotengeneza na kuuza
pombe kama masoko yatakayoleta
faida. Imeripotiwa kwamba shughuli
za kibiashara za sekta ya pombe
zinaongezeka katika nchi za Kiafrika,
na kwa sababu hiyo, madhara
yanayotokana na utumiaji pombe
yanatarajiwa kuongezeka. Isitoshe,
kwa kuwa utumiaji pombe unaripotiwa
kuongezeka pale kipato cha watu
kikiongezeka, nchi ambazo zina
uchumi unazidi kukua zina uwezekano
mkubwa wa kuathirika sana.
Ushahidi wa madhara ya utumiaji
pombe umekuwa ukizidi kuibuka
ndani ya mwongo uliopita kutoka
tafiti zilizotumia taratibu bora za
utafiti. Madai kwamba kuna faida
fulani kutokana na kutumia pombe
zimepitwa na wakati, kwani tafiti
za hivi majuzi zimekadiria kwamba
maradhi yanayotokana na utumiaji
pombe duniani yanaongezeka kadri
utumiaji pombe unavyoongezeka. Sera
za kitaifa zinafaa kuzingatia ushahidi
huu uliopatikana kutokana na utafiti.
Ni hatua gani zinazochukuliwa kote
duniani ili kutunza afya ya jamii,
na kuna mipango gani ya siku za
mbele?
Ili kulinda watu dhidi ya madhara ya
pombe, ni muhimu kukusanya data
kuhusu kiasi cha utumiaji pombe
kwa watu binafsi, na data hizi zinafaa
kuzingatiwa wakati wa kutunga sera za
kudhibiti pombe.
Shabaha namba 3.5.2 ya Malengo ya
Maendeleo Endelevu (SDGs), ambayo
inalenga kiasi cha utumiaji pombe
cha kila taifa, inahitaji ufuatiliaji
wa utumiaji pombe. Shida inaibuka
katika shabaha hii kwenye nchi zenye
makundi makubwa ya watu wengi
wasiokunywa pombe na ukosefu
wa data kuhusu kiasi cha utumiaji
pombe cha watu binafsi. Katika hali
hii, wakati wa kuhesabu kiasi cha
wastani cha utumiaji pombe, hesabu
inayozingatia utumiaji wa jumla wa
watu nchini huzingatiwa. Hali hii
huwa haitoi picha halisi ya kundi
kubwa la wasiokunywa pombe, hasa
wanawake, data zinazopatikana huwa
zinapotosha. Hii ni sababu mojawapo
inayoifanya pombe kutofikiriwa kuwa
chanzo cha hatari katika nchi zenye
kundi kubwa la wasiokunywa pombe.
Sababu nyingine ni kuhusisha utumiaji
pombe na misingi ya kidini na kisiasa,
na hivyo kutoa taarifa nyeti kuhusu
utumiaji pombe wa watu binafsi.
Katika jamii ambazo kunywa pombe
ni marufuku kwa wengi, kwa mfano
nchini Uturuki, ukubalifu wa sera za
kuhakikisha watu hawatumii pombe
lazima zijadiliwe kwani “wachache
wasiokunywa watachangia ongezeko
la utumiaji wa kiwastani”. Basi, utafiti
waweza kulenga kukusanya data
za wasiotumia pombe na sababu za
kutoitumia, pamoja na data za utumiaji
wa hatari.
Ingawa pombe si mada nyeti ya
utafiti kwa jumla, inaweza kuwa nyeti
kulingana na mazingira na utamaduni,
na kwa hiyo kuwahitaji watafiti
kuandaa tafiti zao kwa uangalifu. Pia,
tofauti na uvutaji sigara, utafiti wa
utumiaji pombe huhitaji utaratibu
Mahojiano na: Fatıma Aydın
PROFESA MSHIRIKI,
DAKT. TORUN:
“ULIMWENGU
UMEKUBALI MADHARA
YA POMBE”
Ni mtaalam wa afya ya jamii na pia
mwana academia ambaye anafanya
kazi nchini Uturuki. Ni mwanamke
ambaye amekuwa akiongoza Utafiti
wa Tathminiya Sera wa shirika la
Kimataifa la Kudhibiti Pombe wa
Uturuki tangu mwaka 2016.
PROFESA MSHIRIKI, DAKT. PERİHAN TORUN
44