

Yeşilay’dan
Bağımlılıkla
Mücadelede
Eğitim Seferberliği
Shirika la Afya Duniani (yaani; WHO) limeutambua uraibu wa michezo ya
kubahatisha kama ugonjwa, na kuipa michezo hiyo, nambari ya utambuzi
ya Uainishaji wa Kimataifa wa Magonjwa yaani, ICD. Tulizungumza na Dkt.
Daniel Spritzer, Mratibu wa Bodi ya Wakurugenzi wa Jumuiya ya Kimataifa
wa Uchunguzi ya Ukuaji wa Tabia (ISSBD), kuhusu uraibu wa michezo
ya kubahatisha na tishio linalojitokeza kwa watoto na vijana, na kuhusu
maendeleo yake yaliyoshuhudiwa kote ulimwenguni.
Je, ni nini hali ya Dunia ya sasa ya
teknolojia na uraibu wa michezo ya
kubahatisha?
Tunaishi katikadunia inayotawaliwasana
na teknolojia kiasi kwamba teknolojia
hiyo huathiri jinsi tunavyowasiliana na
kuishi na wenzetu, jinsi tunavyojifunza
na pia tunavyojiburudisha. Uelewaji
wa vipengele vya kiafya na madhara ya
tabia zinazobadilika haraka haraka ni
changamoto kwa wataalam bingwa wa
Afya ya Akili.
Tangu
miaka
ya
tisini,
watafiti
wamekuwa wakichunguza kwa makini
uongezekaji na tatizo la kucheza
michezo ya mtandaoni na tafiti nyingi
zimefanywa kitika nchi kadhaa duniani
kote, wakikusanya ushahidi ambao
umewezesha kuwepo kwa maendeleo
makubwa katika uwanja huu.
Kwa sasa, jamii ya kisayansi ya kimataifa,
Afya ya akili na serikali wametambua
kwamba michezo ya mtandaoni pamoja
na mambo ya kimtandao kama vile
mitandao ya kijamii na ponografia
vinaweza kuathiri watumiaji wake kiasi
cha kuitwa ugonjwa wa akili.
Ni Kitu gani ambacho kinafanywa
kulinda afya ya jamii na kuna mpango
gani kwa wakati ujao?
Kuingizwa kwa uraibu wa michezo ya
kubahatishakatika toleo la 11 la Uainishaji
wa Kimataifa wa Magonjwa yaani ICD-11
wa Shirika laAfyaDuniani, kunawakilisha
hatua muhimu sana inayofaidi afya ya
jamii. Kwa kutoa mfumo unaothibitisha
ushahidi
unaoongoza
taratibu
za
utambuzi wa ugonjwa zinazohusiana
na hali hii, inawezesha na kuhalalisha
upataji wa huduma, zikichochea pia
utafiti wa kisayansi.
Ni muhimu hapa kueleza wazi wazi
tofauti kati ya “michezo ya kubahatisha”
na “Uraibu ya michezo ya kubahatisha”.
Michezo ya kubahatisha ni shughuli kuu
ya burudani ya watoto wengi, vijana na
watu wazima, na inachukua jukumu
kubwa katika elimu, afya na utamaduni.
Uraibu wa michezo ya kubahatisha ni
pale ambapo michezo ya kubahatisha
imekuwa
shida
na
kusababisha
maadhara kwamaisha ya kila siku, jambo
ambalo hutokea kwa idadi ndogo sana
ya wachezaji. Kuanzisha hatua za kuzuia
hali hii kunaweza kuwa na ufanisi bila
kuathiri tabia ya kawaida (yaani, kukuza
utumiaji salama huku ukiongeza faida za
shughuli hii maarufu na ya kupendeza)
ni changamoto kwa wadau wote.
Je! Jukumu la Mashirika yasiyo ya
Serikali ni ipi katika suala hili?
Utumiaji wa teknolojia haujihusishi
na kitengo mahsusi cha elimu, au
kujihusisha na utaalamu wa taaluma
moja. Vivyo hivyo, Uraibu wa michezo
unaweza kueleweka kwa njia tofauti
na wadau wengi tofauti (wahusika wa
michezo na familia zao, tasnia, mfumo
wa afya na elimu, waandishi wa habari,
wasomi, na serikali).
Mashirika ya kijamii yasiyo ya serikali
yanaweza kuchangia pakubwa katika
mapambano dhidi ya uraibu wa michezo
ya kubahatisha kwa kuhamasisha
jamii kuhusu athari za michezo ya
kubahatisha, kwa kuanzisha mikakati ya
kijamii ya kuzuia uraibu, na kwa kuunda
njia za ubunifu kulingana na picha ya
kuaminika ya kile kinachohitajika. Hii
itaruhusu mashirika yasiyo ya serikali
kuwahudumia watu walio hatarini zaidi,
na kutoa habari muhimu kuhusu jinsi
wanavyoweza kusaidiwa.
Je, una Maoni gani kuhusu
mapambano ya Green Crescent dhidi
ya uraibu?
Mapambano ya Green Crescent dhidi
ya kila aina ya uraibu huelekezwa na
mtazamo ambao unahusu watu na
ushahidiNi shirika la kipekee duniani
kwa sababu ya jihudi zake. Miradi ya
kuzuia uraibu ambayo ilianzishwa awali
nchini imeenea pole pole katika nchi
nyingi duniani. Kupitia miradi hii, Green
Crescent, ina uwezo mzuri sana wa
kusaidia watu walio na tatizo la uraibu
wa kucheza michezo ya kubahatisha
na familia zao kwa kuihamasisha jamii
kuhusu suala hilo na kwa kutoa huduma
za matibabu na ukarabati na pia kupitia
utetezi na ushirikiano kamili.
Mahojiano na: Sara Evli
Uraibu wa michezo ya
kubahatisha ni pale ambapo
michezo ya kubahatisha
imekuwa shida na
kusababisha maadhara kwa
maisha ya kila siku, jambo
ambalo hutokea kwa idadi
ndogo sana ya wachezaji.
DKT. DANIEL SPRITZER;
“MICHEZO YA KUBAHATISHA YA
MTANDAONI NI “UGONJWA”
IKIATHIRI MAISHA YA BINADAMU”
Dkt. Daniel Spritzer ni Daktari wa
Akili wa Watoto na vijana huko Porto
Alegre, Brazil. Yeye yuko katika Bodi
jamii ya Kimataifa ya Uchunguzi
wa Uraibu wa Tabia yaani (ISSBA)
amekuwa mratibu wa kundi la watafiti
kuhusu uraibu wa tekinolojia-kundi
lilioundwa to kuchunguza namna
uongezekaji wa kutumia mitandao
ya kijamii unavyoathili afya ya akili
ya watoto na vijana tangu mwaka wa
2006.
DKT. DANIEL SPRITZER NI NANI?
40