

AZIMIO LA KIMATAIFA LILOFANYWA NA
“MPANGO WA KUJITUMA WA ISTANBUL”
GREEN CRESCENT
K
atika hafla iliyoandaliwa na Green
Crescent, wawakilishi wa Mashirika 21
yasiyo ya Kiserikali kutoka nchi 15 tofauti
mkiwemoUswidi, Ghana, Italia naMarekani,
walikutana tarehe 12-13 mwezi wa Juni.
Kutokana na mkutano uliofanyika katika
makao makuu ya Green Crescent katika
kioski ya Basketmakers huko Istanbul,
mpangompya uliwekwa katikamapambano
dhidiyauraibunamadawayakulevya.Wakati
wa mkutano, mashirika yanayoongoza
katika uwanja wa upambanaji na uraibu wa
madawa walijadiliana na kutoa maoni na
mapendekezo. Ilisisitizwa kwamba, hatua
za haraka haraka za dunia nzima zinapaswa
kuchukuliwa kushughulikia uraibu wa
madawa kwa sababu ya afya na ustawi wa
binadamu wote.
Katika tamko la pamoja, Mashirika
yasiyo ya Kiserikali yalisema “Acheni
utumiaji wa dawa za kulevya”
Katika kikao cha kwanza cha mkutano
huo, utakaofanyika huko Istanbul kila
mwaka, viongozi wa maoni ya umma katika
mapambano dhidi ya uraibu wa madawa
duniani kotewaliundampangowakimataifa
na kuandaa “Azimio la Kujituma la Istanbul”.
Likiwa na vifungu 15, tamko hilo liliwataka
viongozi wote wa maoni kutoka kwa
makundi mbali mbali, yakiwemo michezo,
afya, vijana na biashara, kubadili hali ya
kijamii ili kuzuia matumizi ya dawa za
kulevya na kujenga jamii zenye afya njema.
Tamko hilo pia lilithibitisha umuhimu wa
mifumo ya utunzaji inayolenga kuwaokoa
waraibu na kutoa hatua kamili, kuanzia
uokoaji mapema hadi upunguzaji wa hatari
yauraibu, nakutokakwaukarabati hadimtu
kuwa pona akaanza kusishi na binadamu
wengine. Kwenye mkutano na waandishi
wa habari uliofanyiwa katika mkutano huo,
Ripoti ya madawa ya kulevya 2019 ya Kituo
cha Ufuatiliaji wa Dawa za Ulaya na vile vile
ilishughulikiwa.
Wawakilishi waMashirika 21 yasiyo ya
Kiserikali kutoka katika nchi 15
Hotuba ya ufunguzi wa hafla hiyo ilitolewa
na Wakili Osman Baturhan Dursun, Katibu
Mkuu wa Green Crescent, ikifuatiwa na
maoni kutoka kwa viongozi mashuhuri
kamaRaiswa IOGTKristinaSperkovakutoka
Uswidi; Mwanzilishi na Rais wa KKAWF
Cristina Von Sperling Afridi kutoka Pakistan;
na Boro Goic wa RUN kutoka Bosnia na
Herzegovina. Mbali na Green Crescent,
wawakilishi wa asasi zinazoongoza katika
mapambano dhidi ya ulevi, kama vile;
CADCA, CADFY, Drug Policy Futures, , EURAD,
FORUT, IOGT, KKAWF, RUN, San Patrignano,
SCAD, mfuko wa pesa kwa ajili ya kutoa
msaada wa Sunny Trust, VALD, VNGOC na
WFADwalihudhuriaMkutanowa Kwanzawa
kujituma wa Istanbul.
Green Crescent: wanaongoza katika
mapambano dhidi ya uraibu wa madawa
duniani”
Kufuatia mkutano huo, Meneja Mkuu wa
GreenCrescent Sultan Işık alifanyamkutano
na waandishi wa habari pamoja na Kristina
Sperkova, Cristina Von Sperling Afridi na
Boro Goic na kujadiliana kuhusu tamko hilo
lililoandaliwa na makubaliano ya kawaida,
na kutoa habari zaidi juu ya Mpango wa
Istanbul.
Akisisitiza
kwamba
Green
Crescent
imekuwa ikifanya kazi na majukumu
muhimu tangu miaka ya 2000, Işık alisema
kwamba: Kupitia vituo vyetu vya Mafunzo
na Ushauri vya Green Crescent (YEDAM),
vinavyolenga kutoa suluhisho kwa matatizo
yanahusiana na uraibu wa madawa kwa
watu wetu, na ambayo hutoa huduma za
bure zamsaada wa kisaikolojia kwa waraibu
wamadawa na familia zao, matunda bora ya
kazi za Green Crescent yamesambazwa kote
nchini. Idadi ya vituo ambavyo vimeingia
katika huduma nchini Uturuki inaongezeka
kwa kasi. Kupitia Vituo vyetu vya Ushauri
vya Green Crescent tunawaisaidia vijana
wetu na familia zao, na tunajitahidi kuunda
hadithi za kimafanikio kuhusu matibabu ya
uraibu wa madawa na kujumuishwa kwa
watu wengine kwenye jamii.“
Green Crescent imeongoza uundaji wa mpango wa Istanbul katika jaribio la kuungana na mashirika yenye
nia sawa duniani kote katika juhudi za kuzuia uraibu, kuunda njia mpya na kuunda mkakati wa dunia. Katika
hafla ambayo iliandaliwa na Green Crescent, wawakilishi wa Mashirika 21 yasiyo ya Kiserikali (NGOs)
yanayoongoza duniani kote walitia saini tamko la pamoja na kupambana na uraibu wa dawa za kulevya.
42