

K.B., ambaye maisha yake yalikuwa hatarini baada ya kuanza kucheza
mchezo mwovu wa simu unaowaomba wachezaji wake kufanya
majukumu ya kujiumiza; jukumu la mwisho likiwa ni kujinyonga,
unaojulikana kwa umaarufu kama Blue Whale aliokolewa na Kituo cha
Mafunzo na Ushauri cha Green Crescent yaani (YEDAM) muda mfupi
tu kabla ya kukamilisha jukumu la hatari la mwisho. K.B., aliweza
kushikilia na maisha akagundua kipaji chake cha upakaji rangi/uchoraji,
shukrani kwa mafunzo ya kimaendeleo aliyoyapata katika Kituo cha
Mafunzo na Ushauri cha Green Crescent yaani (YEDAM) . Kwa sasa K.B.,
anaingojea kwa hamu siku ile ya maonyesho ya uchoraji.
K.B. ni kijana ambaye maisha yake
yalihatarishwa sana kwa sababu ya
kutawaliwa na uchezaji wa mchezo
mwovu wa simu ujulikanao kama
Blue
Whale;
mchezo
unaowamba
wachezaji wake kujiumiza na mwishowe
kujinyonga. Yeye alianza kucheza
mchezo wa Blue Whale akiwa na miaka
17, akitimiza majukumu aliyopewa
kwenye zana tumizi (App) ya simu yake
yamkononi. Alipoingia ndani yamchezo
huo siku baada ya nyingine, majukumu
aliyopewa kutimiza yalikuwa hatari sana.
Mara nyingi, K.B alipanda juu ya jengo
ili aruke lakini akaogopa kulitekeleza
jukumu hilo. Kwa wakati huu uokozi wa
K,B.ulianza, akielekezwa na daktari wa
familiakwaKituochaMafunzonaUshauri
cha Green Crescent yaani (YEDAM).
Katika mahojiano na mwanasaikolojia,
kutoka Kituo cha Mafunzo na Ushauri
cha Green Crescent yaani (YEDAM),
akiwa ameogopa na mwenye haya, K.B.
alielezea alivyoingiliwa na kutawaliwa
huko. : “Nilishutuka sana nilipopoteza
kazi yangu kwa sababu ya ugonjwa wa
ubongo” Baada ya kupoteza kazi, upweke
ulinivamia. Kwa bahati mbaya, karibu
nilikuwa sina rafiki yeyote. Mchezo
ulikuwa kama dawa kwangu. Nilikuwa
nikipoteza muda wangu na kuhisi
kana kwamba nilikuwa nikiwasiliana
na kitu. Kwa asili, nilianza kuchukua
muda wangu wote nikicheza mchezo
nikaingizwa katika kizingia hiki”.
Kukataa kutekeleza jukumu la hatari
Licha ya kutaka kuuachiliambali mchezo
wa Blue Whale, na kuufuta kutoka
simu yake mara kadhaa, K.B. hakuweza
kuacha kucheza mchezo huo. Angeufuta
mchezo huo lakini aupakue mara
nyingi kwa taharuki ya kutaka kujua
jukumu litalofuata.Kwa kufuta maagizo
aliyopewa na mchezo, KB alinyoa nywele
zake zote nakuiparura mikono yake.
Alipowaamini Wataalamwa saikolojiawa
Kituo cha Mafunzo na Ushauri cha Green
Crescent yaani (YEDAM) ilikuwa rahisi
kuongea kuhusu maagizo yalitolewa
mchezoni na kujipumzisha kidogo. KB
alileta mfuko uliojaa vodonge ambavyo
vilikuwa ni vya kutumia kutekeleza
mojawapo wa majukumu. K.B alisema
pia kwamba alikwenda juu ya nyumba
akiwa na nia ya kuruka lakini alikuwa
ameogopa.
Kuadhimisha maonyesho ya uchoraji
Awali ya yote, Kituo cha Wataalam
wa akili Mafunzo na Ushauri cha
Green Crescent walimfahamisha K.B.
kuhusu hatari za mchezo huo, ingawa
ilikuja kufahamika kwamba nia ya
mchezo huo ilikuwa kuumiza watu.
Walimwambia K.B. kwamba wasimamizi
wa mchezo huo waliweza kuwaona
wale wanaoucheza kupitia kamera ya
simu na kwa hivyo walikuwa wanajua
walichokuwa wakifanya. Kwa idhini ya
K.B. kamera zambele za simu zilifunikwa
kwa kutumia utepe namchezo ukafutwa.
Kwa kusindikizwa na wanaseikolojia K.B.
alienda kwa Kituo cha Daktari wa familia
mara tena. Daktari walichunguza anuani
ya mgonjwa kutokana na kumbukumbu
za taarifa za mgonjwa na kuwajulisha
polisi. Daktari wa Kituo cha familia
alimrejesha kwa hospitali ya Magonjwa
ya akili ya Erenköy Katika mchakato
huu wote K.B. aliendelea kushirikiana na
Kituo cha Mafunzo na Ushauri cha Green
Crescent akagundua kipawa cha sanaa
katika uchoraji wakati wa mafunzo.
K.B. alianza kuhudhuria vipindi katika
kituo cha mafunzo na ushauri cha Green
Crescent kwa siku tatu au nne kila wiki ili
kukuza kipawa chake kipya cha uchoraji
na sasa anaingojea siku atakapoanzisha
maonyesho ya ubinafsi ya uchoraji.
KUOKOLEWA NA GREEN
CRESCENT KWA MCHEZO
MWOVU WA SIMU WA
KUJINYONGA WA BLUE
WHALE
31