

kwa mara mipango iliyoandaliwa na
Umoja wa mataifa kwa miaka 3 na
limekuwa mwenyeji wa vikao anuai,
Işık alisema kuwa uraibu sio shida ya
watu wengine, akisisitiza kwamba kila
mtu anapaswa kulishughulikia kwa
kutumia mikakati sawa na kwa unyeti
unaostahili.
“Nchi ya Uturuki ni mfano wa
kuigwa”
Gilberto Gerra, Mkuu wa Kitengo cha
Matibabu ya Kinga na Ukarabati wa
UNODC, alizungumzia juu ya umuhimu
wa uhusiano wa mzazi na mtoto
wake katika kuzuia ulevi wa dawa za
kulevya, akisema kwamba zamani
watoto walikuwa wanapata fursa ya
kukulia katika familia kubwa zilizo na
uhusiano wenye nguvu , jambo ambalo
lilichangia pakubwa katika ukuaji wa
kibinafsi.
Gerra alisema kwamba mtoto ambaye
ana uhusiano mzuri na wazazi wake
atakuwa na tabia njema sana jambo
linalomfanya kuwa sugu zaidi kwa
tabia zote mbaya kutoka nje.
Gerra alisifu kazi ya Green Crescent
akisema, “Nchi ya Uturuki ni mfano wa
kuigwa katika mkoa huu, kwa sababu
ya kazi yake katika uwanja wa madawa
ya kulevya.”
Wakati wa Kikao cha Tume kwa Dawa
za Nakotiki cha mwaka wa 2019,
katuni zilizoibuka washindi katika
Mashindano ya mara ya tatu ya Katuni
ya Green Crescent yalionyeshwa
kwenye jengo la Umoja wa Mataifa
huko Vienna.
Tume ya dawa za kulevya za
Nakotiki ni nini?
Ikianzishwa na Baraza la Uchumi na
Jamii la Umoja wa Mataifa (ECOSOC),
Tume ya Dawa za Nakotiki (CND)
ilizinduliwa ili kusimamia mikataba ya
kimataifa ya kudhibiti dawa za kulevya.
CND inafuatilia hali ya dawa za Dunia,
inakuza mikakati ya udhibiti wa dawa
za kimataifa na kutoa maoni kuhusu
jinsi ya kushughulikia tatizo la dawa
za kulevya duniani. CND hukutana
kila mwaka, na katika mkutano huo
maamuzi muhimu huzingatiwa na
kupitishwa kuhusiana na suala hilo.
Kwa kuongezea, mikutano ya ndani
ya CND hufanywa mara kwa mara
kufuatilia maendeleo duniani, kujua
mpema mbinu itakazotumiwa na
mashirika yasiyo ya Kiserikali na
raia katika uwanja huu na kupitisha
mwongozo wa kisiasa.
Katika mikutano ya mwaka ya
iliyohudhuriwa na Green Crescent,
ilitambuliwa kuwa njia ya kupambana
na shida ya dawa za kulevya
inabadilika.
Wakati
baadhi
ya
Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs)
na nchi zinatetea uundaji wa sera za
kupunguza mahitaji na matumizi ya
dawa za kulevya, mashirika ya NGO
na nchi nyingine zinasema kwamba
katika suala la udhibiti wa dawa za
kulevya, kupunguzwa tu kwa athari
zinazohusiana na dawa kulevya
ndiko kunakopaswa kushughulikiwa.
Katika mikutano ya ndani ya CND,
maoni haya hushughulikiwa mara
kwa mara na mashirika yasiyo ya
kiserikali. Kupitia mikutano hii, Umoja
wa Mataifa unatambua kozi ya shida
ya dawa na mahitaji katika eneo hili.
Jukumu linalodhaniwa na Green
Crescent katika misaada ya CND kwa
ushirikiano wake na Mashirika yasiyo
ya Kiserikali ambayo yanazingatia
kanuni yalizopitisha, na hutumika
kama mwongozo katika kutambua
hatua zinazopaswa kuchukuliwa kwa
udhibiti wa dawa za kulevya.
27