

Huku ikiendelea na mapambano yake dhidi ya uraibu, kama tatizo la kawaida la binadamu, na ikifanya
kazi pia katika uwanja wa urekebishaji, Green Crescent inaweka mfano kwa dunia kupitia utekelezaji wa
vielelezo ambavyo imeunda. Sultan Işık, Meneja Mkuu wa Green Crescent, ambayo imegusa maisha ya
watu wengi kupitia miradi ambayo imefanya nyumbani na ng’amboni, alisema, “Green Crescent ni kiongozi
duniani katika hatua za uingiliaji kati katika uzuiaji, pamoja na urekebishaji.”
Green Crescent ni shirika lisilo
la kiserikali ambalo linaendelea
kutoa huduma katika mapambano
dhidi ya uraibu wa madawa ya
kulevya, wakati pia likifanya kazi
katika uwanja wa urekebishaji.
Je, unaweza kutuambia kuhusu
shughuli za urekebishaji za Green
Crescent?
Uraibu wa madawa ya kulevya ni tatizo
linaloathiri utendaji wa kijamii wa mtu
binafsi, lakini ambalo linahusu jamii
kwa ujumla. Kuongezeka kwa uraibu
wa madawa ya kulevya katika miaka
ya hivi karibuni kumepelekea hali
ambapo tatizo hili limekuwa mojawapo
ya masuala mazito zaidi ya dunia na
kijamii. Kuna mambo mengi ambayo
huwalazimisha watu kuanza uraibu wa
madawa ya kulevya, mkiwemo sababu
za kibaolojia, kiwango cha kiuchumi na
kijamii, mawasiliano ya familia, ufikiaji
wa kiwango fulani cha kielimu, pamoja
na sababu za kiurithi, mambo ambayo
mara nyingi yanahusiana. Kwa mujibu
wa haya, tatizo hili na michakato
ya matibabu inafaa kutathminiwa
kulingana na mitazamo mbalimbali
na kushughulikiwa kwa kushirikisha
vipengele vya ugonjwa vya kimatibabu,
kisaikolojia na kijamii. Kwa hivyo, ni
salama kusema kwamba uraibu wa
madawa ya kulevya ni tatizo ambalo
linahitaji mikabala ya kijumla na
inayohusisha taaluma zaidi ya moja.
Nchini Uturuki, kuna mfumo ambao
unalenga matibabu ili kutatua tatizo
la madawa ya kulevya, na huduma
zinatolewa na Kituo cha Utafiti,
Matibabu na Elimu Kuhusu Uraibu
wa Pombe na wa Madawa ya kulevya
(AMATEM) na Kituo cha Matibabu
ya Matumizi ya Madawa ya Kulevya
miongoni mwa Watoto na Vijana
(ÇEMATEM). Hata hivyo, kushughulikia
tatizo hilo kwa kutumia mtazamo wa
kimatibabu tu hakutoshi ikiwa lengo
ni kukomesha tatizo la uraibu. Mtu
ambaye ameanza kupata matibabu na
ameweza kuepuka uraibu wake mara
nyingi hurejea kwenye mazingira
halisi, mazingira ya kijamii na ya
kisaikolojia ambayo yalimlazimisha
kuanza tabia ya uraibu wa madawa ya
kulevya, na wanaweza wakashindwa
kuhimili majaribu wakaanza kutumia
madawa ya kulevya tena. Kwa mujibu
wa hayo, inafaa tuwaimarishe watu
kisaikolojia,
kuwasaidia
kupata
stadi za kujifunza taaluma fulani,
kuimarisha mahusiano yao ya ndani ya
familia, kuwafanya wahisi thamani ya
maisha yao na kuwasaidia kuendelea
kuishi katika mazingira safi. Utoaji
wa huduma za urekebishaji kwa
watu wenye uraibu wa madawa ya
kulevya ni wa muhimu sana, kwa kuwa
unawasaidia kuchukua hatua za hakika
za kuendelea mbele katika mchakato
wa matibabu yao na kujiepusha
na hali ya kurudi nyuma baada ya
Picha: Semih Akbay
SULTAN IŞIK,
MENEJA MKUU WA GREEN CRESCENT:
“GREEN CRESCENT NI
KIONGOZI PIA
DUNIANI KATIKA
UREKEBISHAJI”
28