

matibabu yao kumalizika. Kwa sababu
hii, tulianzisha Kituo cha Mafunzo na
Ushauri cha Green Crescent (YEDAM),
ambacho hutoa huduma za kisaikolojia
na kijamii kwa watu wenye uraibu wa
pombe na wa madawa ya kulevya,
bila malipo, na sasa tunazindua Kituo
cha Urekebishaji cha Green Crescent
ili kuimarisha uhusiano kati ya
matibabu, urekebishaji, na michakato
ya ujumuishaji wa kijamii.
Mojawapo ya hatua za kwanza kwa
msingi wa mradi zilizochukuliwa na
Green Crescent katika uwanja wa
urekebishaji zilikuwa ni uanzishaji
wa Kituo cha Ushauri cha Green
Crescent. Unaweza kutuambia jinsi
hii ilivyotokea?
Kama
Green
Crescent,
tulikuwa
tunafahamu kuhusu upungufu wa
huduma za urekebishaji na ushauri
zinazopatikanakwaajiliyamapambano
dhidi ya uraibu katika nchi yetu.
Wakati mahitaji ya jamii ya huduma
kama hizo yalipoongezeka, sheria yetu
ndogo ilibadilishwa mnamo mwaka wa
2013 ili kujumuisha urekebishaji ndani
ya upeo wa shughuli zetu. Mnamo
mwaka wa 2015, tulizindua huduma
yetu ya Simu ya Moja kwa moja ya
Kutolea Ushauri, ambayo ingetumiwa
na wataalam wanasaikolojia waliopata
mafunzo katika uwanja huu ambao
wangekuwa tayari kujibu maswali ya
waraibuwamadawa ya kulevya pamoja
na familia zao. Tangu 2016, tumefungua
Kituo cha Green Crescent cha Mafunzo
na Ushauri ambapo tunatoa huduma
za bure za kisaikolojia na kijamii kwa
waraibu wa pombe na madawa ya
kulevya, na tumeunda kielelezo cha
kipekee ambacho kinafaa utamaduni
wetu vizuri. Huduma zinazotolewa na
vituo vyetu zinalenga wateja.
Matibabu yanaendeleaje kwenye
YEDAM? Je, maisha ya mraibu au
jamaa zake hubadilikaje baada ya
kushauriana na YEDAM?
Mmojawapo wa wateja wetu alitutumia
ujumbe akisema, “Asante kwa kufufua
maisha yangu.” Kwa kweli, jibu la
swali lako liko katika maandishi haya.
Maisha ya mraibu au jamaa zake
huanza kubadilika; hugeuka kuwa kitu
kizuri, chenye afya, chenye amani na
maana mara tu baada ya kuwasiliana
na Kituo cha Mafunzo na Ushauri cha
Green Crescent. Hii ni kwa sababu
mraibu na jamaa zake wanakutana
na wanasaikolojia ambao wamepata
mafunzo katika uwanja wa uraibu wa
madawa ya kulevya kwanza, badala ya
kukutana na mtu asiye mtaalamu au
ofisa wa kituo cha kupokea maulizo.
Ningesema hii ni mojawapo ya
huduma muhimu zaidi ya vituo vyetu.
Watu ambao wanawasiliana nasi kwa
simu wanahimizwa kufanya miadi na
kuanza mchakato wa matibabu. Katika
hatua inayofuata, tunaamua njia ya
matibabu kwao inayofaa na tunawapa
rufaa kwa matibabu zaidi, ikihitajika.
Hata wakati wakiwa wanapokea
matibabu katika mashirika haya,
wanaweza kuendelea kupata huduma
za kisaikolojia kutoka kwa YEDAM.
Kwa kweli, tunamshughulikia mraibu
wa madawa ya kulevya kwa ujumla,
pamoja na familia yake, mazingira
ya kijamii, hali ya kiuchumi, kiwango
cha elimu na stadi za mawasiliano.
Wakati tukitoa huduma ya kisaikolojia
na kijamii, tunatembelea familia zao
na kukagua mazingira yao ya kijamii.
Mtejaakihitajikuimarishamawasiliano
na familia yake, tunatoa msaada
kwa familia hiyo katika mawasiliano.
Mara tu wateja wetu wanapofikia
hatua fulani, tunawaelekeza waende
kwenye warsha za Kituo cha Mafunzo
na Ushauri cha Green Crescent
ambacho kina kazi mbili. Kwanza,
tunawahimiza wageni wetu kuanza
kufanya shughuli za kijamii kama
vile kazi za mikono na michezo, na
kuboresha ujuzi wao katika warsha
hizo. Pili, tunawasaidia wateja kupata
Kielelezo cha Kituo cha
Green Crescent cha
Mafunzo na Ushauri
kinaweza kuhamishiwa
na kurekebishwa na nchi
tofauti. Tunakaribisha
ushirikiano wa kimataifa
na tuko tayari kutoa uzoefu
wowote na maarifa ambayo
tumepata katika uwanja wa
urekebishaji.
Shukrani za dhati kutoka kwa mama ambaye
mtoto wake anapata usaidizi wa kuzindua
akili tena katika kituo cha Ushauri cha Green
crescent…
“Asante sana kwa kumsaidia mtoto wangu
kupata heshima yake tena…”
29