

mwezi kwa miezi zaidi ya 1000. Jarida
hili, ambalo hadi sasa lina matoleo
1000, hutoa majibu kuhusu namna ya
kuishi maisha yenye afya, amani na
utulivu, na ushupavu wa kihisia, kifikra
na kimwili, kwa mtazamo tofauti kila
mwezi. Aidha, tumekuwa tukichapisha
jarida la watoto la Green Crescent
“Mavi Kırlangıç” kwa miaka 50 kwa
lengo la kuwaongoza watoto kushikilia
mwenendo wa maisha ya afya, na
kuchangia maendeleo yao ya kifikra.
Pia tunatekeleza miradi na kampeni
nyingi kote Uturuki mara kwa mara
kuhimiza watu kushiriki michezo,
ambayo ni mojawapo ya njia za kuishi
mwenendo wa maisha yenye afya,
kupitia matawi yetu yanayohusiana na
michezo, na tunahitimisha shughuli
hizi kwa kuandaa ziara ya kuendesha
baiskeli ya kila mwaka.
Ninaweza kutaja miradi mingi sana
mingine,lakinihebunitajetuileambayo
ndiyoyamuhimusanabilayakufafanua
kwa kirefu: Mashindano ya Kuonyesha
vipawa ya Kizazi chenye Afya na ujao
wenye afya, sherehe ya tuzo ya Phoenix,
Mashindano ya Kimataifa ya Vigororosi
ya Green Crescent na Mashindano
ya Filamu Fupi, ni tu baadhi ya kazi
tunazotekeleza ili kuwatayarisha raia
wetu kushikilia mwenendo wa maisha
yenye afya, yasiyo na ulevi, kwa lengo la
kunusuru ujao wa watu.
Mbali na kutekeleza tafiti za kutoa
kinga, pia tunatoa huduma za ukarabati
kwa walioelemewa na ulevi pamoja
na jamaa zao. Kupitia vituo vyetu vya
Ushauri vya Green Crescent, tunatoa
msaada wa kutuliza akili za walevi ili
kuwawezesha kufidia miaka ya maisha
waliyopoteza. Kwa kuwa ulevi unaathiri
pia familia na marafiki za walevi,
tunawaingiza pia kwenye mchakato wa
ukarabati na kuzingatia hasa namna ya
kuwawezesha kukubaliwa tena katika
jamii zao.
Shirika la Green Crescent tayari
linatekeleza miradi na shughuli
muhimu sana katika nchi, lakini
pia hutekeleza miradi na kukuza
ushirikiano wa kuendeleza azma
yake ya kupambana na ulevi katika
ngazi ya kimataifa. Twambie juu ya
ushirikiano huu na kazi za Green
Crescent.
Shirika la Green Crescent limezidi
kufikiria swali moja tu tangu
lianzishwe miaka 100 iliyopita: Watu
watawezaje kuishi maisha yenye afya
na yasiyozongwa na ulevi? Kwa azma
hii, tunatumia kila njia kufikia raia
wetu na binadamu wote kwa jumla, na
kuwasilisha ujumbe wetu. Hatutendi
kazi hizi kwenye eneo letu tu au jiji
letu au nchi yetu tu; bali tunazipasha
binadamu wote. Katika muktadha
huu, tumefanikiwa kupewa nafasi ya
kuwa washauri wa shirika la Umoja
wa Mataifa na Baraza la Kiuchumi
na Kijamii. Tukiwa na hadhi hii,
tunapasha uzoefu wetu, tajriba zetu
na ujuzi wetu kwa nchi zote duniani.
Pia huwa tunachangia mara kwa mara
utafiti wa Shirika la Afya la Dunia juu
ya ulevi. Kwa kupasha ujuzi wetu na
uzoefu wetu kwa mashina ya Green
Crescent yanayotenda kazi zake chini
ya mwavuli wa Shirikisho la Kimataifa
la Green Crescent, ambalo linapatikana
katika nchi zaidi ya 60, tunasambaza
kazi zetu kwenda bara nne.
Tunaandaa makongamano, mikutano
na mafunzo mara kwa mara ya
kupigana dhidi ya ulevi, na tunafanya
tahakiki za kichinichini kwa kila zoezi
letu kwa kutumia ushauri na idhini ya
kamati yetu ya Kisayansi. Pia tunafanya
uchunguzi wa kisayansi ili kufanikisha
kazi zetu, na huwa tunapindua miradi
yetu mara kwa mara. Kisha tunapasha
ushahidi wa kisayansi kutoka utafiti
wetu kwa asasi mbalimbali kote
duniani.
Tunaliona tatizo la ulevi kama tatizo
la jamii na binadamu wote. Tunajua
kwamba hakuna nchi au shirika
ambalo linaweza kushinda tatizo hili
peke yake, na kwa hiyo, huwa tunapata
usaidizi kutoka watumishi wa kujitolea
na kupasha habari za tatizo hili kwa
raia wetu, kwa kuwashirikisha kwenye
harakati zetu za kuhakikisha kwamba
raia wetu na binadamu wote wanapiga
marufuku aina zote za ulevi. Tunao
zaidi ya watumishi wa kujitolea 100,000
nchini Uturuki, na jumla ya vyama vya
Green Crescent 120 katika vyo vikuu na
matawi ya Green Crescent katika kila
jiji.
Tunatoa misaada ya kifedha kwa
mashirika
yasiyo
ya
kiserikali
katika
sehemu
mbalimbali
za
Uturuki, ambayo yanashiriki utafiti
unaohusiana na miradi na malengo ya
Green Crescent. Tukizingatia kazi zote
ambazo tumekwisha tekeleza hadi
sasa, inadhihirika wazi kwamba azma
yetu imekuwa ileile kwa karne nzima.
Tutazidi kujitahidi hadi tutakaposhinda
kila aina ya ulevi.
ISSN 1303-3980K.K.T.C. FİYATI 11TL
0D\ÖV
_
6D\Ö
<,/
_
7/
Jalada la 1000 la jarida la Green Crescent
lilipambwa na msanii maarufu İsmail Acar
akiongozwa na kielelezo cha “Ahera na Green
Crescent vyazaliwa kutoka majivu ya ndege
phoenix”
Buğra Çimen, İstanbul
20