

Ulevi unasababisha hatari za kudumu kwa binadamu. Utandawazi
umesababisha mabadiliko katika mienendo ya kimaisha, na
umewezesha upatikanaji wa madawa ya kulevya na teknolojia mpya
za kulevya kwa urahisi zaidi. Kwa kuwa zinasambazwa kwa haraka
sana, harakati za kupigana dhidi ya ulevi zimekubwa na vikwazo
tele. Dakt. Mehmet Dinç ambaye ni Rais wa muda wa Green Crescent
amesisitiza kwamba kwa sababu hiyo, jitihada zaidi zilenge hatua za
kutoa kinga, na aliongeza kwamba “Sisi kama Green Crescent, hadhira
lengwa yetu ni binadamu wote. Tunajitahidi kuhakikisha kwamba
walioelemewa na ulevi wanaweza kujikokota kutoka shida hiyo,
wakati pia tukitoa kinga kwa wale ambao hawajalewa ili wasilewe.
Shabaha yetu ni kuona afya njema na furaha kwa binadamu wote.
Utafiti umeonyesha kwamba licha
ya jitihada kubwa za kupambana
na ulevi ulimwenguni kote, tatizo
hili linazidi kuongezeka. Kwa maoni
yako, jitihada za kupigana na ulevi
zimefaulu kwa kiasi gani, na tafiti
ambazo zimefanywa hadi sasa
zinatosha?
Kwa kuwa ulevi ni jambo linaloathiriwa
na
mambo
kadha,
limekuwa
tatizo kubwa sana ambalo linazidi
kuongezeka duniani. Ongezeko la tatizo
hili kila kuchao haimanishi kwamba
nchi, mashirika, asasi za kiafya na vyuo
vikuu havijishughulishi na utafiti wa
kutosha kuhusu tatizo hili. Kinyume ni
kwamba asasi hizi zimefanya shughuli
baada ya shughuli na kuandaa miradi
kadha wa kadha kwa madhumini ya
kupigana na ulevi. Lakini, kiwango
ambacho tumefikia na habari ambazo
tumekusanya hadi sasa zinaonyesha
kwamba tafiti zilizokwisha fanywa
hazitoshi kulikabili vyema tatizo la
ulevi. Katika ulimwengu wa sasa, ulevi
ni tatizo lenye nyuso mbalimbali na
linalosambaakwakasi tele; kasi ambayo
inakuwa vigumu sana kwa tafiti zilizopo
kustahimili, na mabadiliko baina ya
tafiti hutokea kwa haraka sana.
Una maoni gani kuhusu sababu za
ongezeko la ulevi katika ulimwengu
wa lleo?
Kila
taaluma
imekumbwa
na
mabadiliko ya haraka sana duniani
kote. Kuanzishwa kwa utandawazi
katika maisha yetu kumesababisha
misimamo
ya
kifikra
ya
watu
kudhoofika polepole kwa kufungamana
na mabadiliko ya mienendo ya maisha
kutoka juu hadi chini, na kusababisha
kuvunjika kwa mahusiano baina ya
watu, na mwanzo wa mitafaruko ya
kijamii na matatizo ya kiuchumi. Sasa
ningependa kurejelea mfano mwepesi
sana. Msimamo wa kifikra wa mtu
unapodhoofika polepole, nia yake ya
kushikilia jambo fulani huongezeka.
Makampuni yauzayo vifaa vya kulevya
hulenga haja hii ya mtu, na kuleta vifaa
vya kulevya kwa jamii hizo na kwa watu
kama suluhisho lepesi na la haraka.
Picha zilipigwa na: Halil Altınta
DAKT. MEHMET DİNÇ,
RAIS WA MUDA WA GREEN CRESCENT:
“TUNALENGA AFYA
NJEMA NA FURAHA
KWA BINADAMU
WOTEY”
Alisoma shahada yake ya elimu kwa Idara
ya Masomo ya Ushauri na kutuliza Akili
ya Chuo Kikuu cha Marmara. Alisoma
shahada ya uzamili katika Elimu kutoka
Chuo Kikuu cha RMIT na shahada nyingine
ya uzamili katika masomo ya Saikolojia ya
Kimatibabu kutoka Chuo Kikuu cha Okan,
kisha alipata shahada ya uzamivu kutoka
Chuo Kikuu cha Marmara. Aliteuliwa
kuwa Rais wa Chama cha Washauri wa
Kisaikolojia na Chuo cha Australia nchini
Uturuki. Hivi sasa yeye ni mhadhiri katika
idara ya Saikolojia ya Chuo Kikuu cha
Hasan Kalyoncu. Sasa hivi yeye ni Rais wa
muda wa Green Crescent; pia Mjumbe wa
Bodi ya Chama cha Utamaduni , Jamii
na Familia; na pia wakala wa Uturuki
kwenye Kituo cha Dulwich cha Matibabu
ya Kinathari; na pia wakala wa Uturuki kwa
Chama cha Waliowahi kusoma Cho Kikuu
cha RMIT; na mjumbe wa Bodi ya Ushauri
ya Jarida la Matibabu ya Kisaikolojia na
Tabia za Kiakili na Utafiti.
Ameandika vitabu vitatu vyenye vichwa
İnternet Bağımlılığı, Gençliğe Kitabe na
Psikolojiye Giriş, na pia amekuwa na miradi
ya uandishi wa pamoja na Profesa Dr.
Kemal Sayar. Pia ameandika sura kwenye
vitabu 8.
DAKT. MEHMET DİNÇ NI NANI?
18